Header Ads Widget

HALMASHAURI KIGOMA ZAHIMIZWA USAJILI MAKUNDI MAALUM NeST



Afisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya mji Kasulu Azizi Nurfus (kulia) akitoa taarifa ya halmashauri katika usajili wa makundi maalum katika mfumo wa manunuzi ya umma (NeST)
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Wazo Mwang'onda (Kushoto) akimkabidhi hati Mkurugenzi wa halmashauri ya mji Kasulu Vumilia Simbeye baada ya halmashauri hiyo kuvuka lengo la usajili wa makundi maalum katika mfumo wa NeST
Kiongozi wa mbio za mwenge Wazo Mwang'onda (kushoto) akizungumza na viongozi wa halmashauri ya mji Kasulu mkoani Kigoma na Mamlaka ya udhibiti wa manunuzi ya umma (PPRA) alipotembelea banda la mamlaka hiyo  wakati wa mkesha wa mwenge wa uhuru kwenye halmashauri ya mji Kasulu mkoani Kigoma


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

 Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru 2026, Wazo  Mwang’onda 

amezitaka halmashauri za mkoa Kigoma kuhakikisha zinasajili na  kutoa tenda kwa makundi  maalum ili yaweze kushiriki kwenye mchakato wa manunuzi ya umma  kwa taasisi za serikali  yanayotoka na  asilimia 30 ya bajeti zao za ununuzi za taasisi hizo.

Mwang'onda alisema hayo  wakati wa mkesha wa mwenge wa uhuru katika halmashauri ya mji wa Kasulu

 mkoani Kigoma akieleza utaratibu huo unaongeza wigo wa ajira kwa jamii na kuyapata uwezo makundi hayo kuwa na shughuli za kufanya badala ya kuwa tegemezi

Kiongozi huyo wa mbio za mwenge alizipongeza halmashauri za Mkoa Kigoma kwa kuweza  kufikia na kuvuka  malengo ya usajili wa makundi maalum na 

kusisitiz  kuwa halmashauri za mkoa Kigoma  lazima zizingatie kwamba tenda ambazo hazizidi shilingi milioni 500 zinanatolewa kwa makundi hayo maalum kwani kwa sasa makundi mengi yaliyosajiliwa yameonyesha uwezo wa kutekeleza mpango huo.

Awali Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Kanda ya Kati na Magharibi, Mhandisi Suma Atupele akitoa taarifa  kwa  Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2026, Wazo Mwang’onda   alisema kuwa hadi kufikia Septemba saba mwaka huu

Mkoa Kigoma umefanikiwa kusajili Makundi  maalum 1359   kwenye Mfumo wa manunuzi ya umma  (NeST).

Atupele alisema kuwa pamoja na kupata usajili kwa makundi hayo pia  halmashauri za mkoa huo  zimetoa zabuni zenye thamani ya Zaidi ya shilingi milioni 500 kwa makundi  hayo  yanajumuisha vijana, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu na kwamba idadi hiyo imevuka lengo la mamlaka hiyo la kusajili  makundi maalum 1200 mkoani Kigoma.

Kwa upande wake  Afisa maendeleo ya jamii wa halmashauri ya mji wa Kasulu, Azizi Nurfus alisema kuwa jumla ya makundi maalum 165 yamesajiliwa katika halmashauri hiyo kwenye mfumo wa ununuzi wa kielektroniki (NeST) ambapo kuanzia mwaka 22024/2025 makundi maalum matatu yalipata tenda kwenye halmashauri hiyo zenye thamani ya shilingi milioni 108 kwenye halmashauri hiyo, vikundi viwili vilipata tenda nje ya halmashauri hiyo yenye thamani ya shilingi milioni 253.6 na kikundi kimoja kimepata tenda mbili zenye thamani ya shilingi milioni 74 nje ya mkoa Kigoma.


BONYEZA LINK HII KISHA PIGA KURA ZOTE NNE BAADA YA KUFUNGUA NENDA SEHEMU

BONYEZA LINK HII KUPIGA KURA ZOTE NNE

 IMEANDIKWA PIGA KURA KISHA BONYEZA SEHEMU IMEANDIKWA NDIO


MATUKIO DAIMA MEDIA IMETEULIWA KUWANIA TUZO ZA SKA2026 TUNAOMBA KURA YAKO WAWEZA KUPIGA KURA KIRAHISI KULIKO KUPITIA LINK HII

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI