Header Ads Widget

TANZANIA YANG'ARA KATIKA DIPLOMASIA YA AMANI NA UHIFADHI

 


Tanzania imeendelea kushiriki katika mijadala ya kimataifa kuhusu amani, uhifadhi wa mazingira na nafasi ya vijana katika kuleta maendeleo endelevu, kupitia mkutano wa kimataifa uliofanyika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Mkutano huo  uliwakutanisha zaidi ya vijana 3,000 kutoka nchi 54 za Afrika na nchi 14 kutoka mabara mengine, kujadili nafasi ya vijana katika kujenga amani, usalama na maendeleo ya Afrika.

Tanzania iliwakilishwa na mwanadiplomasia wa masuala ya uhifadhi, Ridhiwani Gambalela, aliyeshiriki mijadala kuhusu diplomasia, mazingira na nafasi ya vijana katika kujenga Afrika yenye amani na ustawi.

Katika mjadala huo, Gambalela alihimiza nchi za Afrika kuongeza juhudi za kumaliza migogoro na kuwawezesha vijana kutumia nguvu, maarifa na ubunifu wao katika maendeleo, uhifadhi wa mazingira na ujenzi wa jamii salama.

Akifungua mkutano huo, kiongozi wa vijana kutoka DRC, Serge Etinkum Anza, amesema vijana wana wajibu mkubwa wa kutumia uwezo wao kutafuta suluhisho la changamoto zinazoikabili Afrika.

“Amesema amani na usalama ni msingi wa maendeleo endelevu, hivyo vijana wanapaswa kushirikishwa kikamilifu katika juhudi za kujenga jamii zenye utulivu,” amesema Anza.

Mwanzilishi na kiongozi wa FIJADA, Jonathan Masuta, pia amesisitiza umuhimu wa kuwapa vijana nafasi kubwa katika ujenzi wa Afrika yenye amani, umoja na maendeleo.

Mkutano huo uliandaliwa na Forum International de la Jeunesse Africaine pour le Développement de l'Afrique (FIJADA) kwa kushirikiana na Serikali ya DRC kupitia Wizara ya Vijana.

Miongoni mwa ajenda katika mkutano huo zilikuwa kuimarisha amani na usalama barani Afrika, kuhamasisha usitishwaji wa migogoro na kuendeleza utekelezaji wa Agenda 2063 ya Umoja wa Afrika.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI