Header Ads Widget

NAIBU WAZIRI MMUYA AONGOZA MBIO ZA HISANI KUHAMASISHA UWEKEZAJI WA MADINI LINDI

Na Matukio Daima Media.

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kasper Mmuya, ameongoza washiriki wa Maonesho ya Madini na Fursa za Uwekezaji Mkoani Lindi kushiriki mbio za hisani zilizolenga kuhimiza wananchi kufanya mazoezi na kujenga afya ya mwili.

Mbio hizo zimefanyika leo asubuhi huko wilayani Ruangwa zikiwashirikisha wawekezaji, wachimbaji, watumishi wa serikali na wananchi wa mkoa huo.

Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mbio hizo, Naibu Waziri Mmuya aliwahimiza wananchi wa Mkoa wa Lindi kuchangamkia fursa za madini zilizopo mkoani humo ili kujikwamua kiuchumi.

Kwa upande wake, Mratibu wa Maonesho ya Madini Lindi, Mwijuma Mkungu, amesema mbio hizo ni sehemu ya mkakati wa kuvutia na kutangaza fursa za madini zilizopo mkoani humo kwa wadau wa ndani na nje ya nchi.


Naye baadhi ya washiriki wa mbio hizo wameeleza kufurahishwa na tukio hilo, wakisema limewasaidia kutambua fursa nyingi zilizopo katika sekta ya madini ambazo hawakuwa wanazifahamu awali.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI