Na Matukio Daima Media.
Uongozi wa Jimbo la Kati Dayosisi ya Meru chini ya Mch. Abel Kaaya Msaidizi wa Askofu Mteule na Mkuu wa Jimbo hilo amesema moja ya mkakati iliyopo katika Jimbo la Kati ni kuhakikisha kunakuwepo na walimu wenye taaluma ya muziki ili kukuza kiwango cha uimbaji na kuondoa changamoto ya kutumia gharama kubwa ya maandalizi ya kwaya kwenye uimbaji.
Akizungumza Sept 20 katika Sikukuu ya vijana na uimbaji Jimbo la Kati, ibada iliyofanyika katika kanisa la KKKT Usharika wa Nshupu, Mch. Abel amesema ili kuwepo na sulihisho la kudumu lazima kuwepo na walimu wa ndani ambao watashirikiana na walimu wengine nje katika ufundishaji wa kwaya kusudi kuiwezesha kwenda kwenye viwango vya juu vinavyohitajika.
Ameongeza kuwa katika kutimiza azma hiyo mpaka sasa wapo walimu 5 ambao tayari wamepelekwa masomoni katika chuo cha thiolojia na biblia Mwika huku kati yao walimu wawili wakiwa ngazi ya diploma na watatu ngazi ya certificate lengo ni kuzisaidia sharika katika muziki bora na wenye viwango.
Akisoma risala katika ibada hiyo Mwenyekiti wa vijana KKKT Jimbo la Kati, Dayosisi ya Meru Hezron Akyo amesema kupitia uimbaji wa miaka miwili iliyopita Idara ya vijana kushirikiana na ofisi ya Jimbo la Kati imefanikiwa kuwa na miradi mbalimbali ikiwemo ufugaji wa Ng'ombe, ambapo pia idaya hiyo imefanikiwa kuhamasisha Idara ya vijana katika sharika nyingine ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudia.
Ameongeza kuwa jumla ya vikundi 14 zimeweza kushiriki zoezi la uimbaji vikiwemo vikundi vya watoto,vijana, wanawake, mchanganyiko pamoja na Ala za kisasa au vyombo moto huku akieleza kuwa kama Idara ya vijana inatarajia kylufanya ziara katika sharika zote za Jimbo la Kati na kuhamasisha vijana kushiriki uimbaji.
Awali akihubiri katika ibada hiyo Mkuu wa Jimbo la Nairobi kutoka nchini Kenya ambaye pia ndiye mgeni rasmi kwenye uimbaji huo Mch. Agness Chomba ameonya waimbaji kutoweka ushindani katika kuimba bali waimbe wakijua wanahubiri injili ya kristo kwa kufundishana na kuonyana, ambapo amesema katika uimbaji ujasiri na kukuza vipawa, ubunifu kunapatika na kuwataka waimbaji kuendelea kukaa nyumbani mwa Mungu huku neno la Kristo likiwa kwa wingi mioyoni mwao.
Uimbaji huo imekutanisha kwaya 14 zikiwa katika makundi 5 kutoka Sharika za KKKT Jimbo la Kati ikiwemo kundi la watoto, vijana, wanawake, mchanganyiko pamoja na kundi la ala za kisasa kwa maana ya vyombo moto.
Katika makundi hayo mwalimu mshauri wa muziki Edward Mollel akiwataka waimbaji kuzingatia mambo kadhaa ambayo huwezesha kwaya kushinda ikiwa ni pamoja na muonekano na mlingano wa kimavazi ikijumuisha sare na majoho, viongozi kuwa na ujasiri wanapokuwa mbele za watu, kuzingatia uingiaji jukwaani , umakini wa waimbaji kwa viongozi wao, kiongozi kujali muda, kufahamu idadi ya mapigo katika wimbo, pamoja na utengenezaji wa ubora wa sauti.



.jpeg)





0 Comments