Na Fadhili Abdallah,Kigoma
Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru mwaka huu Wazo Mwang'onda amezitaka halmashauri za mkoa Kigoma kuweka mazingira mazuri kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi ili kutekeleza dira ya maendeleo ya Taifa katika kuvutia wawekezaji
Mwang'onda alitoa kauli hiyo akiweka jiwe la msingi la kituo cha mafuta cha Remmy katika kijiji cha Nyachenda halmashauri ya wilaya Kasulu kilichojengwa na mwekezaji binafsi kwa Zaidi ya shilingi milioni 500 ambapo albainisha kuwa kuvutia wawekezaji binafsi ni mpango unaosimamiwa moja kwa moja na Raisi Samia ili kuleta maendeleo nchini.
.jpeg)
kiongozi huyo wa mbio za mwenge alisema kuwa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameondoa mikwamo kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi na ndiyo maana kumekuwa na ongezeko kubwa la wawekezaji nchini hivyo halmashauri zinapaswa kuunga mkono juhudi hizo za Rais Samia kuona namna gani Halmashauri zinaweka mazingira mazuri na zinavutia uwekezaji kwenye maeneo yao.
Pamoja na hilo kiongozi huyo wa mbio za mwenge amesisitiza suala la Amani na usalama wa nchi kwani ndiyo njia pekee ambayo inawezesha masuala ya uwekezaji kufanyika kwa tija na kuleta maendeleo kwa wananchi.
.jpeg)
Awali Meneja wa kituo hicho cha mafuta, Neema Razaro akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo alisema kuwa kiasi cha shilingi milioni 518 kinatarajia kutumika hadi kukamilisha mradi huo ambao kwa sasa umefikia asilimia 85 na unatarajia kukamilika mwezi Novemba mwaka huu.
Razaro alisema kuwa uwekezaji huo unaunga mkono wito wa Rais Samia wa kuvutia wawekezaji wa ndani na nje na kwamba kutekelezwa kwa mradi huo kunatokana na ushirikiano waliopata kutoka serikali ya wilaya Kasulu na kuwezesha wao kama wawekezaji wa ndani kutekeleza mradi huo.





0 Comments