Header Ads Widget

WAZIRI KIKWETE ASHIRIKI MAZISHI YA IDDY SWALA, ALIYEKUWA MSAIDIZI WAKE WA KARIBU JIMBONI

 


Na Mwandishi Wetu, Chalinze.


WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Jakaya Kikwete, jana tarehe 14 Agosti 2026 ameungana na wananchi wa Vigwaza, Chalinze Mkoani Pwani kwenye mazishi ya Iddy Swala aliyewahi kuwa Katibu wake wa Jimbo kwa miaka 8.

Mazishi hayo yamehudhuriwa na viongozi wa Serikali, Dini, Vyama vya Siasa na wananchi mbalimbali.

Akizungumza, Waziri Kikwete amesema Swala alikuwa zaidi ya mtendaji. Alikuwa ndugu, mwalimu na nguzo yake.

"Mimi na Swala tumelelewa pamoja tangu utoto. Maisha yangu yote, makuzi na hata uongozi yameshikana na yeye.

Nisingejua kuswali bila Iddy Swala. Yeye ndiye aliyenifundisha kuswali, kusujudu, kupiga goti. Alinifundisha kumpenda Mtume S.A.W na hata kuhudhuria Maulidi," alisema Waziri Kikwete kwa masikitiko.

Ameongeza: 

"Katika  10 ya uongozi wangu, karibu sita hadi saba nimesimama na Swala. Alikuwa mtu wa watu, hakuwa na tabia ya fitina. Aliniunganisha na watu wengi wa Chalinze na ameniachia marafiki wema."

Kwa mujibu wa kaka yake, Abdul Swala, marehemu alikuwa: Mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kushika nafasi kadhaa ikiwemo Mwenyekiti wa UVCCM Bagamoyo, Katibu wa Uchumi na Fedha CCM Bagamoyo, Katibu wa Mbunge Jimbo la Chalinze miaka 8, na alifanya kazi pia kama Muhasibu katika kampuni tofauti nchini.

Miezi miwili iliyopita aligundulika na tatizo la figo. Iddy Swala ameacha mke na watoto. 

Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi. Amina.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI