Header Ads Widget

RIKOLTO YAELEZA MAFANIKIO YA MIRADI NYANDA ZA JUU KUSINI, WANUFAIKA WASEMA MAISHA YAMEBADILIKA

 



Na Samwel Mpogole, Mbeya.


SHIRIKA la Rikolto limeeleza hatua mbalimbali zilizofikiwa kupitia utekelezaji wa miradi yake katika mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, huku wanufaika wakieleza namna programu hizo zilivyowasaidia kuongeza uwezo wa uzalishaji, kuimarisha vyama vya ushirika na kuboresha shughuli zao za kiuchumi.


Miradi hiyo imekuwa ikiwaleta pamoja wakulima, vyama vya ushirika na wadau mbalimbali katika jitihada za kuimarisha mifumo ya chakula, kuongeza thamani ya mazao, kuboresha upatikanaji wa masoko na kuhakikisha wazalishaji wanapata manufaa zaidi kutokana na shughuli zao.


Akizungumza kuhusu utekelezaji wa miradi hiyo, Shukuru Tweve, Mratibu wa Miradi wa Rikolto kwa mikoa ya Nyanda za Juu Kusini, amesema shirika hilo limekuwa likifanya kazi kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuwawezesha wananchi na taasisi zinazohusika na uzalishaji.


Tweve amesema kupitia ushirikiano huo, maeneo mbalimbali yameweza kufanyiwa kazi kwa lengo la kuwajengea uwezo wanufaika na kuwawezesha kukabiliana na changamoto zinazowakabili katika shughuli zao.


Kwa upande wake, Hafsa Mikdadi, Afisa Miradi wa Rikolto, amesema utekelezaji wa miradi hiyo unalenga kuhakikisha wanufaika wanapata ujuzi na uwezo unaoweza kuwasaidia kuendeleza shughuli zao hata baada ya utekelezaji wa miradi.



Amesema moja ya maeneo muhimu yanayozingatiwa ni kuwaunganisha wazalishaji na fursa mbalimbali zinazoweza kuongeza tija na kipato.


Wanufaika wa miradi hiyo wameeleza kuwa ushirikiano kupitia Rikolto umekuwa na mchango katika kuboresha shughuli zao, huku baadhi yao wakisema wamepata maarifa na fursa ambazo awali hawakuwa nazo.


Miongoni mwa wanufaika hao ni Adam Godfrey, Meneja wa Chama cha Ushirika Madibila, ambaye amesema miradi hiyo imekuwa na umuhimu katika kuimarisha uwezo wa chama na wanachama wake.


Godfrey amesema kupitia ushirikiano huo, chama kimeweza kupata fursa mbalimbali zinazosaidia kuimarisha shughuli za wanachama na kuongeza ufanisi katika uendeshaji wa shughuli za ushirika.



Aidha, wanufaika wengine wameeleza namna walivyotumia elimu, mafunzo na fursa walizozipata kupitia miradi hiyo katika kuboresha uzalishaji na shughuli zao za kila siku.



Rikolto imeendelea kusisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya wakulima, vyama vya ushirika, taasisi za Serikali, mashirika na wadau wengine katika kuhakikisha mifumo ya uzalishaji inaimarika na wananchi wanapata manufaa makubwa zaidi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI