Header Ads Widget

MUHIMBILI, DKMA ZAJADILI KUIMARISHA UDHIBITI WA DAWA NA VIFAA TIBA

 


Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Delilah Kimambo, Agosti 11, 2026, amepokea ujumbe kutoka Shirika la Dawa la Denmark (DKMA), ulioongozwa na Ubalozi wa Kifalme wa Denmark nchini Tanzania, kwa ajili ya kujadili na kubadilishana uzoefu kuhusu namna ya kuimarisha udhibiti wa dawa na vifaa tiba.

Katika mazungumzo hayo, Idara ya Famasi ya MNH imewasilisha uzoefu wake katika usimamizi na matumizi salama ya dawa na vifaa tiba, ikieleza mifumo inayotumika katika hospitali inayotoa huduma za kibingwa na ubingwa bobezi.

Majadiliano hayo yamejikita pia katika kuimarisha usimamizi wa mnyororo wa ugavi wa dawa na vifaa tiba, ikiwemo utabiri wa mahitaji, ununuzi, uhifadhi, usambazaji na matumizi sahihi kwa wagonjwa, huku ziara hiyo ikilenga kuweka msingi wa kubadilishana maarifa na uzoefu utakaosaidia kuimarisha mifumo ya udhibiti na matumizi salama ya dawa na vifaa tiba.

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), Dkt. Delilah Kimambo





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI