Header Ads Widget

RC RUVUMA AKUTANA NA KAMANDA WA BRIGEDI YA KUSINI

 


Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, amekutana na kufanya mazungumzo na Kamanda wa Brigedi ya 401 Kanda ya Kusini, Brigedia Jenerali Sijaona Michael Myala, ofisini kwake mjini Songea.

Katika mazungumzo hayo, RC Ahmed amesema usalama wa mkoa ni msingi wa uchumi wa wananchi na taifa kwa ujumla, hasa kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kimkakati inayoendelea katika mkoa na taifa.

Ameeleza matarajio ya viongozi wa mkoa kuwa Kamanda huyo ataendeleza ushirikiano wa karibu na vyombo vingine vya usalama katika kuimarisha ulinzi wa mipaka ya nchi. Akisisitiza kuwa nidhamu, ujasiri na utayari wa kioperesheni ni misingi muhimu ya brigedi hiyo.

Kwa upande wake Brig. Gen. Myala, amewapongeza wajumbe wa Kamati ya Ulinzi kwa uongozi thabiti na usimamizi bora wa masuala ya usalama, hatua iliyowezesha mkoa na maeneo ya mipaka kubaki salama na yenye utulivu.

Ameahidi kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa karibu kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), vyombo vingine vya ulinzi na usalama pamoja na wananchi, ili kuhakikisha ulinzi na amani vinadumu.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI