Habibu Mussa Katibu wa jukwaa la vyama vya siasa mkoa Kigoma
Agripina Buyogera Mwenyekiti wa UWT mkoa Kigoma
Na Fadhili Abdallah,Kigoma
VIONGOZI wa vyama vya siasa mkoa Kigoma wamekemea kauli za wanaharakati ya kutaka kufanya maandamano na kuvuruga Amani kama njia ya kushinikiza serikali kutekeleza madai yao mbalimbali.
Viongozi hao wametoa kauli hiyo katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika mjini Kigoma ambapo wamesema kuwa serikali ipo kwenye mpango mkubwa wa kutekeleza miradi mbalimbali ya kiuchumi kwa wananchi hivyo kufanyika kwa maandamno hayo ambayo yatahatarisha Amani ni adui mkubwa katika uutekelezaji wa mipango hiyo ya serikali.
Katibu wa jukwa la vyama vya siasa mkoa Kigoma, Mussa Habibu alisema kuwa serikali imekubali kufanya mikutano na maridhiano na wadau mbalimbali ili kutekeleza madai yanayoombwa ikiwemo suala la katiba na uhuru wa vyama vya siasa na kwamba anashangazwa kuona wanaotaka kufanya maandamano wakati madai yameanza kutekelezwa.
Kwa upande wake Mjumbe wa baraza hilo, Harun Shahrawi alisema kuwa serikali haikatazi maandamano lakini ni lazima maandamano yajulikane anayeyaandaa na lengo lake lakini kwa haya yanayotaka kufanyika ambayo hayajulikani yataanzia wapi, kwenda wapi na haijulikani atakayeyapokea wala kuwa na kibali ni uvunjifu wa Amani.
Suala la maandamno ya wana harakati limekemewa pia na Mwenyekiti wa Jumuia ya wanawake wa CCM (UWT) mkoa Kigoma, Agripina Buyogera aambaye alisema kuwa Rais Samia na serikali yake yuko kwenye mkakati mkubwa wa kuleta maendeleo kwa watanzania hivyo vurugu na uvunjifu wa a,ani havina nafasi kwa sasa.
Akizungumza katika kikao cha Baraza kuu la UWT mkoa Kigoma kilichofanyika mjini Kigoma Buyogera alisema kuwa kama chama hawaruhusu uvunjifu wa Amani kwani hata nafasi ya chama kusimamia utekelezaji wa ilani hauwezi kufanyika.
Mwisho.







0 Comments