Header Ads Widget

NAIBU WAZIRI SALOME MAKAMBA ASHIRIKI UJENZI KANISA LA ANGLICAN SHINYANGA.

 

Naibu Waziri wa Nishati Salome Makamba ameshiriki ibada na kukabidhi   mifuko 80 ya Saruji katika kanisa la Mtakatifu Stephano Anglican Shinyanga kama sehemu ya kuunga mkono ujenzi unaoendelea katika kanisa hilo.

 Salome Makamba amesisitiza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya kuwajibika kwa jamii na  kukuza umoja wa kitaifa baina ya Serikali, Taasisi za Dini na jamii,huku akiahidi kushiriki kwa kila hatua ili kukamilisha ujenzi wa Kanisa hilo. 

Ameeleza kuwa Taasisi za Dini zinalo jukumu la kusimamia jamii kiimani hatua itakayo waleta watu pamoja,kudumisha amani, umoja na mshikamano ndani ya jamii.

 Akipokea mchango huo Askofu wa Dayosisi ya Shinyanga Johnson Chinyong'ole ametoa shukrani za dhati kwa Naibu Waziri Makamba huku akiweka wazi shauku yake ya kumalizika kwa jengo hilo ili kuruhusu ushiriki mkubwa zaidi na uhuru katika kuabudu kwa waumini wa Kanisa hilo.











Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI