Header Ads Widget

RAIS SAMIA KUZINDUA UJENZI WA SGR, MELI YA Mv.LEMBA KIGOMA

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma


RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajia kufanya ziara ya siku moja mkoani Kigoma Julai 20 mwaka huu ambapo akiwa mkoani humo kiongozi huyo ataweka jiwe la msingi la ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha sita kutoka Tabora hadi Kigoma yenye urefu wa kilometa 506 katika eneo la Katosho mradi 


Waziri wa uchukuzi Profesa Makame Mbarawa  akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Jumapili Julai 19 mkoani Kigoma alisema kuwa Raisi Samia ataweka jiwe la msingi katika hafla  itakayofanyika Eneo la Katosho Manispaa ya Kigoma  Ujiji  mkoani humo ambapo pia atafanya uzinduzi wa  safari za meli ya Mv.Liemba baada ya kufanyiwa ukarabati mkubwa.


Pamoja na hayo Waziri Mbarawa alisema kuwa akiwa mkoani Kigoma Rais Samia atazindua safari za meli nne za mizigo ambazo kila moja ina uwezo wa kubeba mizigo tani 2500 sambamba na kutembelea mradi wa maboresho ya miundo ya bandari ya Kigma.

Mkuu  wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro (kulia) akizungumza kwenye mkutano wa Waziri wa uchukuzi Profesa Makame Mbarawa (katikati) akieleza ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Kigoma Julai 20 mwaka huu


Waziri huyo wa uchukuzi alisema kuwa kwa miradi hiyo ni sehemu ya utekelezaji dira ya maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025/2050 na utekelezaji wake utauweka mkoa Kigoma  kama Lango kuu la biashara kuelekea nchi za maziwwa makuu na kuimarisha usafirishaji wa mizigo katika ushoroba wa kati kupitia ziwa Tanganyika kuelekea nchi za ukanda wa maziwa makuu .



Kwa upande wake Mkuu wa mkoa Kigoma,Balozi Simon Sirro alisema kuwa ujenzi wa reli ya SGR na meli kwenye ziwa Tanganyika zitarahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka bandari ya Dar es Salaam kuelekea nchi za maziwa makuu kwani kwa sasa kumekuwa na changamoto kubwa ya mizigo kuchukua muda mrefu kutoka Dar es Salaam kuwafikia wateja.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI