TAZAMA VIDEO LIVE BOFYA LINK HII
Moto mkubwa umezuka usiku huu wa Ijumaa, Julai 3, 2026, katika Mtaa wa Lumumba, katikati ya Jiji la Mwanza, na kuteketeza maduka kadhaa huku juhudi za kuudhibiti zikiendelea.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, moto huo ulianza majira ya saa mbili usiku kabla ya kusambaa kwa kasi katika eneo la biashara, na kusababisha uharibifu mkubwa wa maduka pamoja na mali zilizokuwa ndani yake.
Hadi sasa, idadi kamili ya maduka yaliyoathirika na thamani ya hasara iliyosababishwa bado haijafahamika, huku vikosi vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji vikiendelea na operesheni ya kuuzima na kuzuia usisambae kwenye majengo mengine ya jirani.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Said Mtanda, amewasili eneo la tukio na kuongoza operesheni hiyo kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama, vikiwemo Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji pamoja na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Chanzo cha moto huo bado hakijabainika, na mamlaka husika zinatarajiwa kutoa taarifa rasmi kuhusu chanzo, kiwango cha uharibifu na hatua zinazofuata mara baada ya uchunguzi kukamilika.






0 Comments