Header Ads Widget

KILIBA: WANAFUNZI WATALINDA AMANI, HAWATASHIRIKI MAANDAMANO

 

Na Hamida Ramadhan,Matukio Daima Media Dodoma


Rais wa Taasisi ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu Tanzania (TAHILISO), Geofrey Kiliba, amesema wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya ufundi stadi Tanzania Bara na Zanzibar hawatashiriki maandamano yanayotarajiwa kufanyika Julai 7, akisisitiza kuwa wataendelea kulinda amani ya nchi huku wakitafuta ufumbuzi wa changamoto zao kupitia mazungumzo na ushirikiano.


Kiliba ameyasema hayo leo mjini Dodoma wakati akitoa tamko la Seneti kufuatia Kikao cha 39 cha Seneti ya TAHILISO kilichoongozwa na Mwenyekiti wa Seneti.


Amesema Seneti imepitisha azimio la kuwataka wanafunzi kuendelea kuwa watulivu, kuheshimu sheria za nchi na kutojihusisha na maandamano yanayoweza kuvuruga amani na utulivu wa taifa.

“Tunatoa wito kwa wanafunzi wote wa vyuo vikuu na vyuo vya ufundi stadi Tanzania Bara na Zanzibar kuendelea kuwa watulivu, kulinda amani ya nchi na kutoshiriki maandamano yanayoweza kuvuruga utulivu wa taifa,” amesema Kiliba.

Aidha, Kiliba amesema TAHILISO imeandaa maombi maalumu yatakayowakutanisha wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya ufundi stadi nchini kwa ajili ya kuliombea taifa na kumuombea Rais Samia Suluhu Hassan ili aendelee kupewa afya njema, hekima na busara katika kuliongoza taifa, pamoja na kudumisha amani, umoja na utulivu nchini.


Aidha, amesema Seneti ilijadili changamoto mbalimbali zinazowakabili wanafunzi wa elimu ya juu, ikiwemo madai ya wanafunzi wa fani za afya kutozwa fedha wakati wa mafunzo kwa vitendo (field), pamoja na masuala yanayohusu Bodi ya Mikopo 


Amesema TAHILISO itaendelea kushirikiana na mamlaka husika katika kutatua changamoto hizo, na kwamba baada ya kikao hicho viongozi watakutana na Wizara ya Afya pamoja na Wizara ya Elimu ili kuhakikisha wanafunzi hawakwami katika mafunzo yao kwa vitendo.


Amesisitiza kuwa TAHILISO itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wa elimu kutafuta suluhisho la changamoto za wanafunzi kupitia mazungumzo na njia za kisheria.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI