Header Ads Widget

WALIOSHINDWA KURIPOTI JKT WAPEWA FURSA NYINGINE

 



Na Hamida Ramadhan, Matukio Daima Media Dodoma


JESHI la Kujenga Taifa (JKT) limewapa fursa nyingine vijana waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT kwa mujibu wa sheria mwaka 2026 lakini wakashindwa kuripoti katika makambi waliyopangiwa kutokana na sababu mbalimbali, kwa kuwataka waripoti katika makambi yaliyo karibu na maeneo wanayoishi.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Mkuu wa Tawi la Mafunzo la JKT, Brigedia Jenerali Peter Mnyani, amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha vijana wote waliochaguliwa wanapata nafasi ya kushiriki mafunzo hayo.


"Vijana wote waliochaguliwa kujiunga na mafunzo ya JKT lakini hawakuripoti katika makambi waliyopangiwa kutokana na sababu mbalimbali wanatakiwa kuripoti katika makambi ya JKT yaliyo karibu na maeneo wanayoishi," amesema.


Amesema vijana hao watapokelewa katika Kambi ya Ruvu JKT mkoani Pwani, Kambi ya Makutupora JKT mkoani Dodoma na Chuo cha Uongozi cha JKT (CUJKT) kilichopo Kimbiji, Dar es Salaam.


Kwa mujibu wa Brigedia Jenerali Mnyani, amesema zoezi la kuripoti litafanyika kuanzia Juni 12 hadi Juni 15, 2026.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI