Header Ads Widget

VIONGOZI WA SERIKALI WAIPONGEZA TAFORI KWA KUSOGEZA HUDUMA ZA UTAFITI KARIBU NA WANANCHI


Dodoma.

 Banda la Taasisi ya Utafiti wa Misitu Tanzania (TAFORI) Juni 22, 2026 limepokea viongozi mbalimbali wa Serikali, akiwemo Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Juma Selemani Mkomi, Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Utumishi, Mhe. Regina Qwaray (Mb), Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), Dkt. Eblate Mjingo,   pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW), Prof. Philipo Lonati Sanga.

Katika ziara hiyo, viongozi hao walipata elimu na maarifa kuhusu fursa za kiuchumi zinazopatikana katika sekta ya misitu na nyuki kupitia matokeo ya utafiti pamoja na kujionea huduma za kitafiti na kidijitali zinazotolewa na TAFORI. 

Aidha, wameipongeza taasisi kwa mchango wake katika kuzalisha maarifa, ubunifu na kutoa majibu ya changamoto mbalimbali katika sekta za misitu na nyuki, jambo linalochochea maendeleo endelevu ya sekta hizo na ustawi wa wananchi.

Viongozi hao pia wameitaka TAFORI kuendelea kupanua wigo wa utoaji wa huduma zake ili kuwafikia wananchi walioko maeneo ya mbali, hususan wale ambao hawajapata fursa ya kushiriki katika maadhimisho haya, ili matokeo ya tafiti na huduma za taasisi yaweze kuwanufaisha Watanzania wengi zaidi.

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanaendelea katika Viwanja vya Chinangali Park, Jijini Dodoma, na yanatarajiwa kuhitimishwa Juni 23, 2026 chini ya kaulimbiu isemayo:





*_“Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu.”_*

#WikiYaUtumishiWaUmma2026 #TAFORI #UtafitiKwaMaendeleo

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI