Header Ads Widget

TAMASHA LA UTAMADUNI WA UJIJI KUHAMASISHA VIVUTIO VYA UTALII KIGOMA


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

Uhamasishaji jamii kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii mkoani Kigoma unaelezwa kuwa moja ya mambo yatakayopewa kipaumbele katika Tamasha la utamduni wa watu wa Ujiji linalotarajia kufanyika kwa siku mbili kuanzia juni 21 mwaka huu.

Mkuu wa Historian na Mali kale wa Taasisi ya Ujiji Heritage and Developoment Hamisi Hababi alisema hayo katika mkutano na waandishi wa habari akieleza kufanyika kwa tamasha hilo nan a kubainisha kuwa mkoa Kigoma umejaaliwa kuwa na vivutio vingi vya utalii ambavyo wakazi wa mkoa huo bado hawajajitokeza kwa wingi kuvitembelea.

Alivitaja vivutio hivyo kama hifadhi ya Taifa ya Gombe na Mahale maarufu kwa uhifadhi wa sokwe mtu, kituo cha Kumbukumbu ya Dk.David Livingstone, njia ya kati ya utumwa kutoka Kigoma hadi Kwihara na vivutio vingine vilivyopo ndani ya mkoa huo ambapo utalii wa ndani haujafanyika wa kutosha.

Pamoja na hilo alisema kuwa tamasha hilo litawaleta pamoja wazazi  na vijana kuzungumzia changamoto zinazosababisha kuporomoka kwa maadili katika eneo la Ujiji na kubainisha kwamba Ujiji imekumbwa na changamoto kubwa ya kuporomoka kwa maadili hivyo kuacha mila na tamaduni za maisha ya watu wa Ujiji kuachwa.

Tamasha hilo litakalofanyika uwanja wa michezo wa Kawawa Ujiji Mjini Kigoma pamoja na mambo mengine litakuwa na maonyesho ya mambo mbalimbali ya asili ya Ujiji ikiwemo vyakula na mavazi ambapo pia mikutano na makongamano yatafanyika kuzungia maendeleo ya mila na tamaduni za eneo hilo sambamba na changamoto zinazojitokeza na kufanya mila hizo na desturi kuachwa.

Akizungumza katika mkutano huo Mjumbe wa kamati ya utendaji ya Taasisi hiyo, Iddi Rajabu Mvano alisema kuwa katika tamasha hilo pia wamealika watu mbalimbali maarufu akiwemo Mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Star, Sunday Manara.

Mvano alisema kuwa  wakati wa tamasha hilo michezo mbalimbali na mbio fupi zitafanyika, ngoma za asili za makabila ya Ujiji na kutembelea maeneo mbalimbali waliokuwa wakiishi watu mbalimbali waanzilishi wa mji wa Ujiji, majengo ya kale, visima vya maji na namna ya maisha ya jumla ya watu hao.

Mwisho.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI