Na Fadhili Abdallah,Kigoma
MKUU wa mkoa Kigoma Balozi Simon Sirro amewataka viongozi na waajiri mahala pa kazi kuona umuhimu wa kulipa mafao na stahiki za watumishi kwa wakati sambamba na kulipa michango ya watumishi hao kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwani jambo hilo lina mchango mkubwa katika kuwafanya watumishi kufanya kazi kwa bidi na kujtuma.
Balozi Sirro alisema hayo wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mei Mosi yaliyofanyika kimkoa wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma na kusema kuwa iwapo stahiki na maslahi ya wafanyakazi yanalipwa kwa wakati inaongeza chachu katika utendaji kazi wa watumishi hao.
Sambamba na hilo Mkuu huyo wa mkoa amewataka wafanyakazi wa serikali na watumishi wa umma mkoani Kigoma kutumia muda wao mwingi katika kutimiza wajibu katika kuwatumikia watanzania kwa misingi ya utu,staha na kuzingatia maslahi ya taifa badala ya kutumia muda mwingi wa kazi kufanya shughuli zao binafsi huku akiwataka wafanyakazi na watumishi wa umma wanapodai haki yao wakumbuke kutimiza wajibu kwa mujibu wa sheria za utumishi.
Akizungumzia maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa yamewekwa mahsusi na serikali ili kupokea kero na changamoto za wafanyakazi na kutafuta namna ya kuzitafutia ufumbuzi akibainisha kuwa zawadi zinazotolewa kwenye maadhimisho hayo zina mchango mkubwa katika kuwafanya watumishi kuongeza juhudi na kujituma huku akitaka uchaguzi wa wafanyakazi bora ufanywe kwa haki kwa kuzingatia vigezo.
Awali akisoma risala ya wafanyakazi mkoa Kigoma katibu wa Chama cha wafanyakazi wa serikali za mitaa (TALGWU) mkoa Kigoma, Johnson Muyomba ameiomba serikali kusimamia na kutafuta mwoarobaini wa utaoondoa changamoto ya wajiri hasa sekta binafsi na za umma kutowasilisha michaango ya wafaanyakazi wao katika mifuko ya hifadhi ya jamii.
Sambamba na hilo Muyomba aliiomba serikali kufanyia marekebisho sheria ya utumishi wa umma ili kuondoa mkanganyiko uliopo kati yake na sheria ya ajira na mahusiano kazini suraa ya 366 (marejeo ya 2019) kuhusu uwasilishwaji wa migogoro ya kikazi katika Tume ya usuluhishi na uamuazi na mahakama kuu divisheni ya kazi.








0 Comments