Mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2026 umeridhishwa na Kasi ya uendelevu wa Mradi wa barabara ya kiwango cha lami yenye urefu wa Mita 600 unaotekelezwa Katika mtaa wa Bohari Kata ya Mwenge Manispaa ya Lindi wenye thamani ya zaidi ya milioni 466
Mradi huo umewekwa jiwe na kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2026 Wazo Mwang'onda Leo mei 2 2026
Akizungumza mara baada ya kuweka jiwe la msingi Katika Mradi wa barabara ya Bohari Mwang'onda amewapongeza tarula kwa usimamizi mzuri wa Mradi huo ambao kuchochea shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo.
Awali akisoma taarifa mbele ya kiongozi huyo wa mbio za mwenge wa Uhuru mwaka 2026 Meneja wa TARURA Wilaya ya Lindi Mhandisi downson Paschal Alisema Mradi huo unaotekelezwa kwa fedha za Mfuko wa Mafuta ambapo Utekelezaji wake umefikia asilimia 90
Amesema mkandarasi anayetekeleza mradi huo ni kampuni ya SEC ya Mtwara, ambapo ujenzi ulianza Septemba 20, 2024 na unatarajiwa kukamilika Mei 28, 2026. ukiwa na lengo la kuboresha miundombinu ya usafiri na kuchochea shughuli za kiuchumi kwa wananchi wa eneo hilo.
Ameongeza kuwa hadi sasa kazi mbalimbali zimekwisha kufanyika ikiwemo kusafisha eneo la barabara, kujenga tabaka la msingi pamoja na uwekaji wa mifereji na makalavati ili kuhakikisha barabara hiyo inadumu kwa muda mrefu.
Aidha amebainidha kuwa kukamilika kwa mradi huo kutasaidia kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa, kupunguza changamoto ya vumbi pamoja na kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi kwa wakazi wa Kata ya Mwenge wa Uhuru na maeneo jirani.
Baadhi ya wananchi wa Manispaa hiyo ya Lindi wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha za maendeleo ya miundombinu, huku wakibainisha kuwa hatua ambayo imeendelea kusaidia kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi kwa wananchi.








0 Comments