Header Ads Widget

MAZISHI YA MWANDISHI WA HABARI EDITHA KARLO NI SIMANZI TUPU KIGOMA


Mtoto wa kwanza wa Mwandishi wa habari Marehemu Editha Karlo aliyekulikana kwa jina la Irene akisoma wasifu wa marehemu wakati wa ibada ya mazishi ya Mwandishi huyo wa habari ambaye amezikwa Mei 2 katika kijiji cha Munyegera wilaya ya Buhigwe  mkoani Kigoma
Familia ya Mwandishi wa habari Editha Karlo wakati wa mazishi ya Mwandishi huyo


Mathias Kanali Mwakilishi wa Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari nchini akitoa salam za umoja huo wakati wa ibada ya mazishi ya Mwandishi wa habari Editha Karlo yaliyofanyika kijiji cha Munyegera wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma
Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari mkoa Kigoma Jacob Ruvilo na Katibu wa chama hicho Mwajabu Hozza wakitoa salam za chama hicho wakati wa ibada ya mazishi ya Mwandishi Editha Karlo yaliyofanyika kijiji cha Munyegera wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma
Watoto wa Mwandishi wa habari wa matukio Daima mkoa Kigoma Marehemu Editha Karlo wakiweka mashada ya maua wakati wa mazishi ya  mwandishi  yaliyofanyika kijiji cha Munyegera wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma
Elius Odhiambo Mume wa Mwandishi wa habari wa matukio Daima mkoa Kigoma Marehemu Editha Karlo  Karlo akitoa heshima wakati wa kuaga kwa mwandishi huyo muda mfupi kabla ya mazishi yaliyofanyika kijiji cha Munyegera wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma

 Baba Mzazi wa Mwandishi wa habari wa matukio Daima mkoa Kigoma Marehemu Editha Karlo Mzee Henry Karlo akitoa heshima wakati wa kuaga kwa mwandishi huyo muda mfupi kabla ya mazishi yaliyofanyika kijiji cha Munyegera wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma


MWANDISHI EDITHA KARLO AZIKWA, WENGI WAMLILIA


Na Fadhili Abdallah,Matukio Daima Media ,Kigoma

Mwandishi wa habari Marehemu Editha Karlo amezikwa kijijini kwao Munyegera  wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma Mei 2 mwaka.

Editha  alifariki dunia April 29 mwaka huu nyumbani kwao Kasulu mkoani Kigoma baada ya kuugua pingili za mgongo kwa muda mfupi ambapo alipata matibabu katika hospitali mbakinbali nchini.

Katika mazishi yaliyofanyika kijiji cha Munyegera wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma  yaliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiongozwa na waandishi wa habari kutoka chama cha waandishi wa habari mkoa Kigoma (KGPC).

Akizungumza katika ibada ya mazishi ya Marehemu Editha Kaimu Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa habari mkoa Kigoma,Jacob Ruvilo alisema kuwa chama hicho na tasnia ya habari mkoani Kigoma imepata pigo kwa kuondokewa na mwandishi huyo wa habari ambaye alikuwa na mchango mkubwa kwenye masuala ya utendaji lakini pia alishiriki kwa karibu kwenye mambo mbalimbali ya kijamii.

Kwa upande wake Mwakilishi wa Umoja wa vilabu vya waandishi wa habari nchini (UTPC),Mathias Kanali alisema kuwa Umoja huo umepokea kwa masikitiko makubwa msiba wa mwandishi huyo kwani alishiriki kwenye miradi mbalinbali ya uandishi wa habari za uchunguzi na uandishi wa habari wenye malengo unaozingatia maslahi ya umma.

Awali akitoa maneno ya faraja wakati wa ibada ya mazishi Mchungaji wa kanisa la Anglikan kanisa kuu wilaya ya Kasulu, alisema kumbukumbu ya maisha ya marehemu Editha itabaki kwa ndugu,jamaa na marafiki waliobaki lakini mapenzi ya Mwenyezi Mungu yametimizwa ambapo ameomba watu wote kuishi kwa kutenda mema na kumuogopa Mungu.

Akizungumza kwa niaba ya Familia Mume wa Marehemu, Elius Odhiambo aliwashukuri watu wote waliotoka nje na ndani ya mkoa Kigoma walioshiriki mazishi hayo na faraja waliyotoa kwa familia na kwamba kifo cha marehemu kimekuwa pigo kubwa kwao kama familia.

Marehemu Editha Karlo aliyezaliwa mwaka 1985 na kumaliza Diploma ya uandishi wa habari kutoka chuo cha Uandishi wa habari Dar es Salaam (DSJ) na kufanya kazi kwenye vyombo mbalimbali nchini  ameacha watoto watatu.

Mwisho.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI