MATUKIO DAIMA MEDIA
MAKETE.Mkuu wa Wilaya ya Makete Mheshimiwa Kissa Gwakisa Kasongwa leo Mei 06, 2026 amezindua na kukabidhi hundi ya mfano ya utoaji wa Mkopo wa 10% kwa vikundi 21 vya Wanawake (11), Vijana (05) na Watu wenye Ulemavu (05 ) wenye thamani ya TSH. Milioni 345.6 .
Katika mkopo huo Wanawake wamepewa TSH. Milioni 180, Vijana Milioni 125.4 na Watu wenye Ulemavu TSH. Milioni 40.2
Mhe. Kissa amesema lengo la serikali kutoa mkopo huo ni kuinua na kuwawezesha kiuchumi na kujiajiri Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu ili kupitia wao wakawe chachu ya kuajiri watu wengine.
Pia ameagiza Halmashauri kuwatambua zaidi watu Wenye Ulemavu ili kuongeza idadi ya Wanufaika katika kundi hilo.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Makete Mheshimiwa Mfamasia Rabson Anton Mahenge amesema kama Halmashauri wataendelea kusimamia miradi ambayo inatekelezwa kupitia fedha hizo za mikopo ya 10% ili kuhakikisha Fedha hizo zinatumika kwenye malengo yaliyo kusudiwa.
Aidha amewataka wanufaika hao kutotumia pesa hizo kulipa madeni waliyonayo kwenye vikundi vya kausha damu ( Umiza ) kwani sio lengo la Halmashauri na serikali kwa Ujumla.
Pia Mwenyekiti wa CCM - Makete Comred Clemence Mwawite ameipongeza Halmashauri kwa kuendelea kuinua uchumi wa Makete kupitia mikopo hiyo ya 10% ambayo inasaidia kwa kiasi kikubwa watu wenye mitaji midogo.
Mbali na hilo ameipongeza Halmashauri chini ya Mwenyekiti Mahenge na Mkurugenzi Jerry D. Mwaga kwa kusimamia vizuri wataalam kwenye makusanyo ya mapato ya ndani kwani kupitia Makusanyo hayo Jamii inapata faida ya kunufaika Mikopo sambamba na kuboresha Huduma mbalimbali za Kijamii ikiwemo Shule na Zahanati .
Kwa upande wa Baadhi ya Wanufaika wa Mkopo huo akiwemo Akrin Ndelwa kutoka kata ya Mbaladze wamesema wanaamini Fedha hizo zitawasaidia kujiinua kiuchumi kwani wilaya hiyo ina fursa mbalimbali za kuwekeza.


.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)





0 Comments