14 Aprili 2026
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania kupitia Kituo cha Uzalishaji wa Mbegu Bora za Miti na Vipando Morogoro, kwa kushirikiana na Unganisha Environmental Conservation(UECO) pamoja na wananchi wa mtaa wa Kilongo, kata ya Mkundi, wamefanikiwa kupanda miti 1,000 katika eneo linalozunguka Mlima Mguruwandege.
Miti iliyopandwa ni aina ya mikangazi na mizambarau pori, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuimarisha uhifadhi wa mazingira ya mlima huo na maeneo yanayouzunguka.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Mhifadhi Samwel Swalo aliyemwakilisha Mhifadhi Mkuu wa kituo hicho, alieleza kuwa lengo kuu ni kulinda vyanzo vya asili, kuzuia uharibifu wa mazingira pamoja na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi.
Aidha, wananchi walipatiwa elimu kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazingira na kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa miti iliyopandwa ili kuhakikisha inaleta matokeo chanya kwa kizazi cha sasa na kijacho.











0 Comments