Shindano la Waongoza watalii lijulikano kama (Safari Field Challenge 2026) lililoandaliwa na Tanzania Tour Guide Foundation, @tzguideawards limeanza kwa kishindo tarehe 8/4/2026 ndani ya Hifadhi ya taifa Ziwa Manyara, Shindano hilo lime lenga kuwajengea uwezo waongoza watalii katika kutoa Huduma bora kwa wageni.
Kwa niaba ya Kamishna wa Uhifadhi TANAPA, Kamishna msaidizi wa Uhifadhi Kitengo cha Maendeleo ya Biashara Jully Bede Lyimo aliwakaribisha washirki hao na kuwahamasisha kuvifahamu na kuvitangaza vivutio na mazao ya utalii yanayopatikana kwenye Hifadhi za Taifa Tanzania.
Aidha, Kamishna Jully amesema kuwa Shindano hilo ni jukwaa muhimu la kuendelea kuhamasisha matumizi ya TanapaGo App katika taarifa za vivutio na maeneo ya uwekezaji yaliyopo ndani ya Hifadhi za Taifa Tanzania, pia amewahamasisha kupigia kura jumla ya Hifadhi za Taifa 10 zilizoteuliwa kuwania tuzo za utalii duniani kwa bara la Afrika 2026.
Washiriki hao ambao ni waongoza watalii waliofika fainali katika shindano hilo wameanza Shindano hilo katika Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara na baadae wataelekea Hifadhi ya Taifa Serengeti, pia wamepata fursa ya kufurahia mazao ya utalii kama vile canopy walkway, canoeing na utalii wa gari mchana (Day Game Drive) na utalii wa usiku (Night Game Drive)
#SafariFieldChallenge #DestinationTanzania #TTGF #AzamTv












0 Comments