Header Ads Widget

RAIS BIYA AMTEUA MWANAE KUWA MAKAMU WAKE

 


Rais wa Cameroon Paul Biya, amemteua mwanae Franck Emmanuel Biya, kushika wadhifa wa Makamu wa Rais, nafasi ambayo imeanzishwa upya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1972.


Hatua hiyo imekuja kufuatia mabadiliko ya katiba yaliyoongeza nguvu ya nafasi ya Makamu wa Rais, ikiwemo jukumu la kurithi moja kwa moja uongozi wa nchi endapo rais atafariki, atajiuzulu au atashindwa kutekeleza majukumu yake.


Wachambuzi wa siasa wanaona uteuzi huo kama sehemu ya mkakati wa kumwandaa Franck Biya kuchukua uongozi wa nchi siku zijazo. Hoja hiyo inaongezwa uzito na umri wa Rais Biya, ambaye akiwa na miaka 93, amekuwa madarakani tangu mwaka 1982 na ni miongoni mwa viongozi wakongwe zaidi duniani.


Aidha, taarifa zinaeleza kuwa Franck Biya amepewa pia majukumu nyeti ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama, hatua inayotajwa kuongeza ushawishi wake katika masuala ya kisiasa pamoja na kijeshi.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI