Header Ads Widget

ONYO LATOLEWA DHIDI YA AJIRA HATARISHI


Na Matukio Daima, Morogoro 

SERIKALI kupitia Tume ya kurekebisha Sheria Tanzania imetoa onyo kali kwa wale wanaowafanyisha watu kazi hatarishi, ikibainisha kuwa adhabu yake ni kifungo cha muda mrefu au faini kubwa.

Wakili wa Serikali, Latifa Mustapha, amesema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Morogoro kutoka makundi mbalimbali ikiwemo wazee wa mabaraza ya kata, viongozi wa dini, vijana na watu wenye ulemavu.

Amesema kuwa vitendo vya kuwafanyisha watu kazi zenye madhara vinaathiri ustawi wa jamii na ni ukiukwaji mkubwa wa sheria.

Kwa mujibu wa Latifa, wananchi wanapaswa kuwa mstari wa mbele kuripoti vitendo hivyo ili kuzuia madhara zaidi.

Aidha, wadau walioshiriki mkutano huo wameahidi kushirikiana na Serikali katika kutoa elimu na kupunguza migogoro.



Mkazi wa Morogoro, Bright Sospeter, amesema kuwa elimu hiyo imewafungua macho kuhusu haki zao.


Anasema kuwa jamii inapaswa kubadilika na kuacha tabia ya kufumbia macho vitendo vya ukiukwaji wa sheria.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI