Header Ads Widget

NMB YATOA BILIONI 24 KWA JAMII, YALIPA TRILIONI 2.7 KODI, WAZIRI MKUU AONYA RUSHWA

 



Na Pamela Mollel,Arusha 

Benki ya NMB imetoa zaidi ya shilingi bilioni 24 kwa shughuli za kijamii katika kipindi cha miaka mitano iliyopita (2021–2025), zikielekezwa katika sekta za elimu, afya, mazingira na misaada ya maafa.

Akizungumza kwenye mkutano wa ALAT uliofanyika Arusha, Mkurugenzi wa Uhusiano wa Wawekezaji, Uendelevu na Mawasiliano wa benki hiyo, Innocent Yonazi, anasema benki hiyo pia imeendelea kushirikiana na Serikali katika maeneo mbalimbali ya maendeleo.

Alisema kupitia mifumo ya kidijitali na mawakala wake, NMB imewezesha ukusanyaji wa zaidi ya shilingi trilioni 9.8 za mapato ya serikali tangu mwaka 2018.

Aidha, benki hiyo imekuwa mdhamini wa mkutano huo kwa kutoa jumla ya shilingi milioni 170, ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono shughuli za mamlaka za serikali za mitaa.

Kwa upande wake, Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba anasisitiza kupambana na rushwa, akisema vitendo hivyo bado vinakwamisha maendeleo na kudhoofisha utoaji wa huduma kwa wananchi.

Aliwataka viongozi wa serikali za mitaa kuchagua viongozi waadilifu, wachapa kazi na wanaowajibika, watakaoweka mbele maslahi ya wananchi badala ya maslahi binafsi.


Aliongeza kuwa uongozi bora unapaswa kuwa na matokeo chanya kwa wananchi, akisisitiza umuhimu wa uwajibikaji, ufanisi na maadili katika kuleta maendeleo endelevu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI