Header Ads Widget

MELI YENYE USAJILI 101242 YAGONGA MTUMBWI ZIWA VICTORIA.

 


NA CHAUSIKU SAID , MATUKIO DAIMA MWANZA.

MWANZA, Meli yenye namba za usajili 101242, MV Uhuru, imegonga mtumbwi uliokuwa umebeba wavuvi wanne katika Ziwa Victoria, na kusababisha wavuvi hao kuzama majini.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mtafungwa, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa Meli hiyo ya aina ya wagon Ferry Mali ya kenya , inayomilikiwa na kampuni ya Kenya Railways corporation (KRC), ilikuwa imebeba tani 1,200 za makaa ya mawe na ikiendeshwa na nahodha Leonard Omollo, raia wa Kenya.

Ajali hiyo ilitokea Aprili 17, 2026 majira ya saa mbili usiku katika eneo la Mihama, Kata ya Kitangiri, Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, wakati meli hiyo ikiwa safarini kutoka Bandari ya Mwanza Kusini kuelekea Bandari ya Kisumu nchini Kenya.

Kwa mujibu wa taarifa, meli hiyo iligonga mtumbwi wenye namba T 2M116529 unaomilikiwa na Emmanuel Mjarifu Kakuru, uliokuwa ukitumia injini aina ya HP 9.9 (MAA) na ilikuwa imebeba wavuvi Emmanuel Elias, Malindi William, Peter Masanja na Noel Julius.

Baada ya kugongwa, mtumbwi ulipasuka na kupinduka na kusababisha wavuvi wote wanne kuzama majini na Wavuvi wawili waliokolewa huku wawili wakizama.

Aidha Myafungwa ameeleza kuwa hadi kufikia Aprili 20, 2026, mwili wa Peter Masanja umefanikiwa kuopolewa, huku juhudi za kumtafuta mtu mmoja aliyezama zikiendelea kufanywa na vyombo vya uokoaji.

Mtafungwa ameeleza kuwa kuwa meli iliyosababisha ajali hiyo haikusimama baada ya tukio, na jitihada za kuwasiliana na mamlaka za nchini Kenya zinaendelea ili kufanikisha hatua za kisheria.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI