Header Ads Widget

MATUKIO MATATU YA MAUAJI YATIKISA MOROGORO, LIPO LA MZEE KUMCHINJA MKEWE KWA WIVU

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP, Andrew Kantimbo


Na Lilian Kasenene,Morogoro

Matukio DaimaApp 


MATUKIO ya kutisha yaliyoibua hofu mkoani Morogoro, mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 64 anadaiwa kumuua mkewe kwa kumchinja kwa kitu chenye makali na kutenganisha kichwa na kiwiliwili, tukio linalodaiwa kusababishwa na wivu wa kimapenzi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP, Andrew Kantimbo, alisema tukio hilo limetokea Aprili 4, 2026, katika kitongoji cha Mkukuzi Chini, kijiji cha Nyameni wilayani Kilosa.

Alisema mtuhumiwa amekuwa akimtuhumu mkewe kwa muda mrefu kuwa na mahusiano ya nje, hali iliyosababisha tukio hilo la kikatili.

Alieleza kuwa baada ya kufanya mauaji hayo, mtuhumiwa alijaribu kujiua kwa kunywa sumu na kwa sasa amelazwa katika kituo cha afya akipatiwa matibabu chini ya ulinzi wa polisi.

Katika tukio jingine,Kamanda huyo wa Polisi alisema mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 35 anashikiliwa kwa tuhuma za kumuua mchumba wake mwenye umri wa miaka 23 kwa kumkaba koo hadi kufa. Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Misegese wilayani Malinyi, ambapo marehemu alikuwa akifanya kazi katika baa ndogo.

Aidha, RPC huyo alisema chanzo cha tukio hilo kinahusishwa na mgogoro wa kifamilia kati ya wawili hao waliokuwa na mahusiano ya kimapenzi.

Katika tukio la tatu, Kamanda Kantimbo alisema polisi wanamshikilia mwanaume mwingine kwa tuhuma za kumuua mkulima mwenzake kwa nia ya kulipiza kisasi, kufuatia mgogoro wa zamani uliosababisha kifungo jela.

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro limewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutumia njia halali za kutatua migogoro ili kuepusha vitendo vya ukatili vinavyoendelea kuhatarisha usalama wa jamii.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI