Header Ads Widget

MATOEO YA KURA ZA MAONI ISIMANI FREDY VUNJABEI APATA KURA 2,703



TAZAMA FULL VIDEO YA MATOKEO BOFYA LINK HII
Na Matukio Daima Media 

Matokeo ya kura za maoni ndani ya chama chama cha Mapinduzi (CCM) yametangazwa rasmi na msimamizi wa uchaguzi huo mdogo ndani ya CCM Sule Masanguti,kuwa  aliyeongoza ni  Fredy Fabian Ngajiro maarufu kama Vunjabei .

 Vunjabei ameibuka kinara kwa jumla ya kura 2,703, akifuatiwa  Festo Shemu Kiswaga akipata kura 868,huku  Emmanuela Kaganda Mtatifikolo akipata kura 682 na Arif Abri kura 233.


Wakati Dkt Abdalah Lusasi kura 100,Claudia Francis (69), Asakwe Widambe (58) Elias Kazikuboma (52), Eng Sebastian Kiyoyo( 37) , Josephat Masambwa (34), David Komba( 27), Tedson Ngwale (24), Egidy Mkolwe (23),Watende Kiyagi (16) , Dkt Tumain Msowoya ( 15), Lazaro Francis Gwira(10), Thitho Cholobi (9), na Thobias Mwilapwa(5). 


Matokeo hayo yanaonyesha ushindani mkubwa uliokuwepo katika mchakato huo wa kura za maoni, huku wagombea zaidi ya 15 wakishiriki kuwania nafasi hiyo. 

Hata hivyo, Vunjabei ameonyesha nguvu kubwa ya kisiasa kwa kuongoza katika kata nyingi, akiwemo kushinda kwa tofauti kubwa katika maeneo kama Kising’a, Mlenge, Idodi, na Malenga Makali.

Kwa upande wake, Mtatifikolo ameendelea kuonyesha ushindani katika baadhi ya kata ikiwemo Ilolo Mpya na maeneo mengine machache, huku Kiswaga naye akijizolea kura katika kata kadhaa lakini bila kuweza kufikia kiwango cha viongozi wawili wa juu.

Matokeo haya ya kura za maoni yanaweka mwelekeo wa nani anayeweza kupewa ridhaa ya chama kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu ujao japo bado vikao vya juu vya chama ndivyo vyenye uamuzi wa mwisho .

Kwa ujumla, ushindi wa Fredy Vunjabei katika kura hizi za maoni unaashiria kukubalika kwake kwa kiwango kikubwa miongoni mwa wanachama na unaweza kuwa chachu ya ushindani mkali katika uchaguzi mkuu wa Jimbo la Ismani 2026.

Wakizungumza baada ya matokeo hayo kutangazwa  baadhi ya wana CCM waliotia nia Dkt Tumain Msowoya ,Arif Abri na Lazaro Francis Wamepongeza mchakato huo ndani ya chama .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI