Header Ads Widget

IFAHAMU HIFADHI YA TAIFA ARUSHA NA UPEKEE WAKE.

 

Na,Mwandishi wetu :Arusha

Hifadhi ya Taifa ya Arusha imeendelea kuwa kivutio muhimu cha utalii nchini, huku idadi ya watalii wanaotembelea eneo hilo ikiongezeka kutokana na vivutio vya kipekee vinavyopatikana ndani ya hifadhi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari katika hifadhi hiyo,Afisa Mwandamizi wa Uhifadhi kitengo cha Utalii ANAPA,Jerome Boniface Ndanzi amesema hifadhi hiyo ni miongoni mwa hifadhi 21 zilizopo nchini na ni hifadhi kongwe ikiwa ni hifadhi ya pili kuanzishwa mnamo mwaka 1960 huku hifadhi ya kwanza ikiwa ni Serengeti.

Jerome amesema hifadhi ya Arusha ni hifadhi ambayo ni muhimu katika Jiji la Arusha,ikiwa na umbali wa kilomita 30 kutoka barabara kuu ya Arusha Moshi, kutokana na upekee wake wa vivutio vilivyomo hifadhi hiyo pia imekuwa ni geti la kuingia katika hifadhi nyingine za Taifa.

Miongoni mwa vivutio vilivyomo ndani ya hifadhi hiyo ni Mlima Meru ambao ni maarufu duniani kwa kuwa Mlima wa tano kwa ukubwa barani Afrika,pia ni Mlima ambao una vivutio vingi ambapo mgeni atakapo panda katika Mlima huo anaweza kujionea vivutio vingine ambavyo hawezi kuvipata katika milima mwingine ikiwemo wanya,maporomoko ya maji pamoja na mandhari nzuri ambayo ipo kwenye hifadhi hiyo.

Kivutio kingine katika hifadhi hiyo ni maziwa yaliyomo kama ziwa momela ambayo yapo ndani ya hifadhi ya Taifa Arusha ambayo yameipendezesha hifadhi hiyo kutokana na uwepo wa ndege jamii ya flamingo ambao wamekuwa wakiyapamba maziwa hayo,hivyo uwepo wa maziwa hayo takribani 7 kumekuwa ni kivutio kikubwa sana katika hifadhi ya Taifa Arusha.


Afisa huyo ameendelea kwa kusema kuwa pamoja na uwepo wa vivutio hivyo pia kipo kivutio cha Kreta ya Ngurudoto au Kasoko ya Ngurudoto ikiwa ni kreta ndogo yenye mandhari nzuri ya kuvutia kutokana na wanyama waliopo ndani ya Kreta hiyo lakini pia imekuwa na maeneo mbalimbali ya sehemu za kukaa wageni na kupata Milo yao na kuona zaidi vivutio vingine vilivyomo ndani ya hifadhi .

Sambamba na hayo hifadhi hiyo imesheheni wanyama mbalimbali kuanzia wanyama wadogo Hadi wanyama wakubwa jamii ya tembo ambao pia wamekuwa wakipatikana katika maeneo ya wazi ikiwemo eneo la Serengeti ndogo,vile vile zipo jamii mbalimbali za ndege zaidi ya 400.

Upekee wa hifadhi ya Taifa ya Arusha umejikita katika mti jamii ya mkuyu ambao unayawezesha magari yenye kimo cha tembo kuweza kupita chini yake pasipo shida yoyote ambapo upekee huo umekuwa ukiiweka hifadhi ya Taifa Arusha kuwa ya kipekee zaidi.

Katika hifadhi hiyo pia wapo nyani aina ya Mbega au black and white Colobus monkey, ambao wamekuwa ni kivutio kikubwa na katika hifadhi hiyo nyani hao wamekuwa kivutio kutokana na wao kutowaogopa wanadamu ambapo hifadhi hiyo umeamua kumbeba mnyama huyo kuwa nembo ya hifadhi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI