Header Ads Widget

ASKOFU MUSHENDWA ATAKA MAOMBI KUKOMESHA VITA DUNIANI

 


Na Fadhili Abdallah,Kigoma

WAUMINI wa kikristo mkoani Kigoma wameungana na waumini wengine duniani kote kusherehekea kufufuka kwa mwokozi wao Yesu Kristo huku Askofu wa kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Magharibi Jackson Mushendwa akisema kuwa dunia imekuwa uwanja wa fujo hivyo kuwataka waumini duniani kote kuomba na kusali  ili vita vinavyoendelea maeneo mbalimbali duniani vikome.

Askofu Mushendwa alisema hayo wakati wa ibada ya Pasaka iliyofanyika katika kanisa  la KKKT jimbo la Magharibi Usharika wa jimbo Kuu Kigoma na kusema kuwa kwa sasa duniani imekuwa siyo sehemu salama ya kuishi kwani vita vimesababisha madhira na maumivu makubwa kwa wanadamu.

Kutokana na hilo alisema kuwa kufufuka kwa Yesu Kristo iwe mwanzo wa kuzaliwa kwa mwanzo mpya wa kuiombea dunia na nchii ya Tanzania kuondokana na madhira hayo akieleza kuwa risasi, mabomu na kila aina ya silaha haitamaliza vita duniani bali kufanyika kwa mazungumzo na kukaa meza moja ambapo pande mbili zinazopingana zitaondoa tofauti zao hivyo kuifanya dunia kuwa sehemu nzuri na salama ya kuishi.


Alisema kuwa hakuna dini wala siasa yenye haki ya kutoa uhai wa watoto wasio na hatia kwa namna yeyote ile ikiwemo kufanyiwa vitendo vya kikatili na kwamba ubinadamu unapaswa kupewa kipaumbele na kuzingatiwa na watu wote kwa kupaza sauti bila woga na kumlilia Mungu na kusema vita imetosha na nchi ziwe na Amani.

Baadhi ya waumini wa kanisa hilo akiwemo Amos Mkumbo waliwatakia wakristo wengine heri ya pasaka huku wakiungana na Askofu wa kanisa hilo, Jackson Mushendwa kukemea vita na mapigano yanayoendelea maeneo mbalimbali duniani ambavyo vimeongezeka hofu na mahangaiko kwa watu wengi. 


Naye Teddy Dawson alisema kuwa machafuko yaliyotokea nchini kwetu Oktoba 29 mwaka jana ni mambo ya kuumiza sana kutokana na watu wengi kupoteza wapendwa wao hivyo kuungana na Askofu Mushemba kukemea vita vinavyoendelea maeneo mbalimbali duniani akitaka pia waumin kuomba na kusali vita hivyo zisitishwe.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI