Mnakumbuka kipindi ambacho COVID 19 imepamba moto duniani? Basi katika hali ya mshangao Mataifa ya Magharibi wakawaambia Iran kuna chanjo za bure wanataka kuwapa, walichojibiwa ni kuwa wanashukuru ila wao tayari wanazo Chanjo zao zilizotengenezwa na Watu wao.
Kupitia Chuo ambacho wamekilipua jana Marekani kinachoitwa Pasteur Institute ambapo kina miaka zaidi ya 100, kupitia Wanafunzi wao Vyuoni na timu ya Wanasayansi walijufungia Maabara walifanya kazi kubwa na mwaka 2021 wakawa na chanjo yao yenye nguvu sana, walianza kwanza Kujaribishwa Wanyama kisha Viongozi wote wa Taifa hilo ndipo wakafuata Raia.
Jana pia Marekani na Israel wamelipua Maabara yao kubwa ambayo inafanya tafiti za dawa za Ganzi pamoja na kutengeneza dawa za kutibu Saratani wameipiga Jana na Iran wanasema ujuzi upo kichwani watajenga tena.







0 Comments