Na Anold Deogratias Matukio Daima Media
Mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Mhandisi Jonstone Mutasingwa kwa kushirikiana na wazazi na walezi wa shule ya msingi Bunena wamenunu mashine ya kudurufu mitihani (photocopy Mashine) yenye thamani ya shilingi milioni 3.4, ili kurahisisha shughuli za kudurufu mitihani katika shule hiyo.
Akizungumza wakati wa kupokea mashine hiyo mkuu wa shule ya msingi Bunena Devotha Mugisha ameeleza kuwa wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule hiyo walichangia kiasi cha shilingi milioni 2 na laki 2 na mbunge wa jimbo la bukoba mjini akaongezea kiasi cha shilingi laki 7, huku uongozi wa kata ukichangia shilingi laki 5.
Aidha mkuu huyo wa shule ameeleza kuwa kununuliwa kwa mashine hiyo itakuwa msaada mkubwa kwa shule katika kurahisisha shughuli za kuchapisha mitiani hivyo kukuza kiwango cha ufaulu katika shule hiyo.
“mashine hii ni muhimu kwetu kwani itasaidia kuinua ufaulu na kurahisisha kuchapisha mitihani hivyo kuondokana na kuandika ubaoni na nichukue nafasi hii kuwashukuru wazazi kwa mchango wao na pia mhembunge kuongezea kiasi kilichosalia”
Kwa upande wake katibu wa mbunge Hamada Simba amesema kuwa mbunge wa jimbo hilo ataongezea kompyuta 2 kwa ajili ya kuchapisha mitiani na pia ameahidi kuendelea kushirikiana na wazizi na walezi wa wanafunzi wa shule hiyo katika kuboresha taalum ya shule hiyo.
“mheshimiwa mbunge atanunua kompyuta mbili ili kuchapisha mitiani na pia ataendelea kushirikiana nanyi katika kuinua taaluma ya shule hii kwa kuchangia mahitaji ya shule yetu”
Naye diwani wa kata ya Bakoba Shabani Rashidi amewataka wazi na walezi wa wananfunzi wa shule hiyo kuendelea kushirikiana na uongozi wa shule katika kuimarisha taaluma ya shule hiyo kwa kushiriki matukio muhimu ikiwemo kuchangia chakula shuleni.
“niwaombe wazazi na walezi tuendelee kushirikiana na uongozi wa shule katika kuboresha taaluma ya wanafunzi wetu kwa kuchangia chakula na pia niwashukuru kwa kujitolewa kuchangia mashine hii mmefanya jambo jema”
Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo Berenado Jovin na Ajela Mswadiku wameshukuru uongozi wa shule, wazazi na mbunge wa jimbo hilo kwa kuwanunulia mashine hiyo ambayo wamesema itasaidia kuinua ufaulu wao.


.jpeg)





0 Comments