Na Lilian Kasenene, Morogoro Matukio DaimaApp
KAMATI ya kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imetoa maelekezo kwa Serikali kuhakikisha inaendelea kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya sekta ya Mifugo ili mazao ya mifugo yaweze kuwa na thamani zaidi kwenye soko la kimataifa.
Mwenyekiti wa kamati hiyo ya kudumu ya Bunge Deo Mwanyika alitoa maelekezo hayo wakati wa ziara ya kamati hiyo wilayani Mvomero, ambapo ulifanyika uzinduzi wa zoezi la utambuaji na chanjo kwa Mifugo.
Mwanyika alisema zoezi hilo la chanjo kwa mifugo ni endelevu na linahitaji fedha nyingi hivyo serikali itoe fedha hizo kwa wingi.
"Sisi kama kamati kazi yetu ni kwenda kuomba Serikali itoe hela kwa wingi na kwa haraka zaidi ili jambo linaloenda kifanyika maana tumeona manufaa, katika zoezi la utambuaji na chanjo kitaifa tunaonekana tumefika asilimia 65.8 kutokana na fedha zilizotolewa,"alis ma.
Alisema la muhimu zaidi kwa Wilaya ya a Mvomero, kwa takwimu ya zoezi hilo kwa ng'ombe wanaotarajiwa kuchanjwa na kutambuliwa ni laki 150 lakini kwa mpaka sasa ng'ombe waliochanjwa ni 15,853 sawa na asilimia 13.
Aidha alisema kuna tathimini ya Halmashauri na Mikoa mingine kufanya vyema moka kufikia asilimia 50, hivyo akaelekeza Halmashauri ya Mvomero kuchukua hatua za ziada na kwamba isione kama zoezi hilo ni la Wizara tu bali walione kama ni wafugaji wao,ili lisaidie wananchi na Halmashauri Ina uwezo wa kupata kodi kutokana na biashara na mazao ya mifugo.
Pia mwenyekiti huyo wa kamati ya Bunge akawashukuru wafungaji kupitia Chama Cha Wafugaji Tanzania (CCWT) kwa mapokeo mazuri,mafanikio na mwitikio mkubwa waliouonyesha.
"Kamati ya Bunge inapotembelea maeneo kama haya tunataka kusikia changamoto zilizopo, wananchi sisi ndio sikio na midomo yenu mna nafasi ya kutwambia waziwazi changamoto mlizonazi lakini mmetoa maneno mazuri ya kutoa dukuduku zenu,"alisema.
Mwenyekiti Mwanyika alisema, kazi zinaonekana na kashuhuda wapo cha muhimu ni kuongeza nguvu ili sekta ya mifugo iweze kutoa mchango kwa mapato ya nchi na ustawi kwa wananchi.
Kwa upande wake Waziri wa Mifugo na Uvuvi Balozi Dk Bashiru Ally Kakurwa, alisema sekta za kilimo,mifugo na uvuvi zimepewa kipaumbela kikubwa katika dira ya miaka ishirini na tano ijayo,ikiwemo suala la usimamizi na uongozi, kushirikisha wafugaji na hiyo imesaidia kufunga mkono jitihada za zoezi la chanjo kwani ilikuwa jipya kwao.
Balozi Dk Kakurwa pia alizungumzia mabadiliko ya mifugo kuwa ni pamoja na afya ya mifugo,lishe ambapo mabadiliko ya tabia nchi iliyosababisha ukame wa muda mrefu na ng'ombe kukonda, malisho na Serikali imetoa ruzuku ya mbegu,miundombinu wezeshi.
"Wizara inawahimiza wafugaji kuwekeza kwenye suala la malisho, mabwawa, majosho na visima vya maji na tuna mpango shirikishi wa kujumuisha wafugaji,jambo lingone ni mitaji kwa wafugaji na tunayataka mabenki na taasisi za kifedha kuwakopesha wafugaji wetu kwani wanakopesheka," alisema.
Katibu mtendaji wa Chama cha wafugaji Tanzania Mathayo Daniel aliiomba Serikali kuendelea kutoa Elimu kwa wafugaji kwani bado baadhi yao hawana uelewa wa kutosha.
Aidha Daniel alisema wao kama wafugaji wa nchi hii wameipokea vyema na imewaokoa kwa kupata faida, kuitambua kupata masoko ya kimataifa na kwamba wafugaji wapo bega kwa bega na Serikali.
"Tunaomba Wizara itutafutie chanjo ya midomo na miguu na kuomba chanjo iwe suala la ratiba, akaomva wafugaji kumilikishwa ardhi kutoka kwenye mashamba yaliyofutwa na Rais,"alisema.
Mwisho.












0 Comments