Header Ads Widget

TANESCO LINDI YAGAWA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI SHULE ZA MSINGI MCHINGA

 


Na Hadija Omary, Lindi.


SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Lindi limetembelea na kutoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wasichana wa Shule za Msingi Umoja na Mchinga Mbili zilizopo Jimbo la Mchinga, Manispaa ya Lindi mkoani Lindi.

 Hatua hiyo ni sehemu ya kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka, kwa lengo la kuunga mkono ustawi na maendeleo ya mtoto wa kike.

Akizungumza kwa niaba ya Shirika la Umeme TANESCO Mkoa wa Lindi Afisa Manunuzi na Ugavi, Anita Patel,  alisema kuwa shirika hilo linaamini katika kurejesha kwa jamii na kusaidia makundi yenye uhitaji maalum, hususan wanafunzi wa kike wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali wakati wa masomo yao.

" Kama Shirika tumeona tusibaki nyuma kuelekea Katika maadhimisho haya ya siku ya wanawake tukaona tuwakumbuke mabinti hawa ili kuwafanya waweze kuudhuria vipindi vya darasani bila kikwazo chochote"




Akizungumza kwa niaba ya shule ya Msingi Umoja  Mwalimu mashauri nasii na Afya alieleza kuwa msaada wa taulo za kike utasaidia kupunguza tatizo la utoro wa vipindi kwa wanafunzi wa kike, hasa wanapokuwa katika siku zao za hedhi. 

Alisema kuwa msaada huo utaenda kufanya nyongeza ya kile ambacho huwa wanafanya kuwanunua taulo kwa ajili ya kuwastili watoto wakike wanaopata dharula wakiwa shuleni

Naye Afisa Ustawi wa Jamii Manispaa hiyo ya Lindi Mariam mghweno aliyetumia fursa hiyo kuzungumza na wanafunzi, aliwakumbusha umuhimu wa kuzingatia usafi wa mwili, kujitambua na kujithamini, akisisitiza kuwa elimu ya afya ya uzazi ni msingi muhimu katika kufikia ndoto zao za kielimu na maisha kwa ujumla.

Kwa upande wao, wanafunzi walilishukuru Shirika la TANESCO kwa msaada huo wakisema umewapa faraja na motisha ya kuendelea na masomo bila hofu wala vikwazo vinavyotokana na changamoto za hedhi. Walisema kitendo hicho ni ishara ya kujali na kuthaminiwa kwa mtoto wa kike katika jamii.









Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI