Header Ads Widget

NAIBU WAZIRI MWINJUMA ATEMBELEA JAB, ASISITIZA UTEKELEZAJI MADHUBUTI WA SHERIA



Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mwinjuma, leo Machi 4, 2026, ametembelea Ofisi za Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) jijini Dar es Salaam ambapo amekukutana na watumishi na kupokea taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya Bodi kwa mujibu wa Sheria ya Huduma za Habari.

Akizungumza katika kikao na watumishi hao, Mhe. Mwinjuma alisisitiza umuhimu wa Bodi kusimamia sheria kikamilifu bila kupepesa, kuhakikisha kanuni zinaimarishwa, kufuatilia na kudhibiti wanaofanya kazi za habari bila ithibati ili kulinda hadhi ya taaluma. 

Mhe. Mwinjuma amepongeza juhudi za Bodi katika kusimamia utekelezaji wa Sheria hadi sasa, huku akisisitiza kuwa haupaswi kulegalega ili kuimarisha weledi, uwajibikaji na imani ya umma kwa vyombo vya habari nchini.

Katika ziara hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa JAB, Wakili Patrick Kipangula, pamoja na kuelezea utekelezaji wa majukumu, amefafanua mafanikio yaliyopatikana katika kipindi cha mwaka mmoja tangu kuzinduliwa kwa bodi ikiwemo uanzishaji wa mifumo ya usajili wa Waandishi, utoaji wa Ithibati na Vitambulisho vya Uandishi (Press Cards), utoaji wa elimu kwa umma, usimamizi wa maadili ya taaluma na uandaaji wa nyaraka zote muhimu za uanzishwaji wa Taasisi chini ya Msajili wa Hazina.

Aidha, kikao kilijadili changamoto zinazoikabili sekta ya habari, hususan uzingatiaji wa maadili katika vyombo vya habari vya mtandaoni na uhitaji wa rasilimali zaidi.






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI