Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera
Mamlaka ya kuzuia na kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) mkoa wa Kagera kwa kipindi cha miezi mitatu (September- Desember 2025) imefanikiwa kuokoa zaidi ya shilingi milioni 57.1 za mamalaka ya mapato nchini TRA katika wilaya ya Missenyi, kutokana na kodi na faini iliyokuwa imekwepwa na baadhi ya wafanya biashara waliongiza bidhaa nchini kutoka nje ya nchi bila kulipia kodi na ushuru wa bidhaa hizo.
Hayo yamebaishwa na mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Kagera Vangsada Mkalimoto wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa majukumu ya taasisi hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu September- Desember 2025, ambapo ameeleza kuwa TAKUKURU kwa kushirikiana na kikosi kazi cha kuzui magendo wilaya ya Missenyi walifanikiwa kukamata magari Matano yakiwemo malori matatu na magari mawili ya abiria yaliyovuka mpaka wa Tanzania na Uganda na vituo vya ukaguzi vya kikodi nchini yakiwa na bidhaa zisizo na vibali na bila kulipa kodi.
“TAKUKURU kwa kushirikiana na kikosi kazi cha kuzui magendo wilaya ya Missenyi tulifanikiwa kukamata magari Matano yakiwemo malori matatu na magari mawili ya abiria yaliyovuka mpaka wa Tanzania na Uganda na vituo vya ukaguzi vya kikodi nchini yakiwa na bidhaa zisizo na vibali na bila kulipa kodi”.
Aidha Mkalimoto ameeleza kuwa baada ya kukamatwa kwa magari hayo wamiliki wa magari hayo wamelipa faini ya magari, mizigo na tozo za serikali kwa Malaka ya mapato nchini TRA, ambapo pia ameeleza kuwa TAKUKURU mkoa wa Kagera itaendelea kuwafuatilia kwa ukaribu watumishi wa umma katika vituo vya ukaguzi wanaofumbia macho ukwepaji wa kodi na upitishwaji wa magendo katika mpaka huo na vituo vya kodi.
“magari hayo yamepatikana na kosa la uingizaji wa bidhaa nchini bila kibali na kutokufuata taratibu zote za uingizwaji wa bidhaa nchini, baada ya kukamatwa kwa magari hayo wamiliki wa magari hayo wamelipa faini ya magari, mizigo na tozo za serikali kwa Malaka ya mapato nchini TRA”
Katika hatua nyingine mamlaka hiyo imefanikiwa kudhibiti ubadhilifu katika ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) katika kituo cha Afya cha kata ya Ngenge wilayani Muleba, ambapo matofali 2,830 yasiyokuwa na ubora yalibainika baada ya kupimwa kwenye vipimo vya kitaalam na hivyo kuonekana hayafai kwa ujenzi wa jengo hilo.
“wakati huo huo TAKUKURU wilaya ya Muleba imefanikiwa kuokoa tofali 2,830 zenye thamani ya shilingi milioni 7.92 katika ujenzi wa jengo la OPD katika kituo cha Afya cha kata ya Ngenge ambayo yamebainika kuwa chini ya ubora unaohitajika na serikali”
Hata hivyo mkuu huyo wa TAKUKURU mkoa wa Kagera amesema kuwa kwa mwaka 2026 mamlaka hiyo itafanya ufuatiliaji wa miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa katika mkoa wa Kagera ili itoe matokeo chanya kulingana na thamani halisi ya fedha iliyotumika.
“TAKUKURU Kagera imejielekeza katika ufuatiliaji wa matumizi ya fedha za serikali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya kimkakati inayotekelezwa mkoani hapa, tutahakikisha miradi hiyo inakamilika kwa ubora wa thamani ya fedha iliyotumika”
Sanjali na hayo TAKUKURU mkoa wa Kagera imewataka watumishi wa umma pamoja na wananchi kuacha kujihusisha na vitendo vya rushwa vinavyorudisha nyuma jitihada za serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi.

.jpeg)
.jpeg)







0 Comments