NA. CHAUSIKU SAID,MATUKIO DAIMA MWANZA.
SERIKALI kupitia Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, imezindua rasmi ugawaji wa mikopo ya Shilingi Bilioni 7 kwa vijana waliopata mafunzo kupitia Programu ya "Jenga Kesho iliyo Bora" (BBT) – Uvuvi.
Hafla hiyo ilifanyika leo machi 7, 2026 Jijini Mwanza, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali kuboresha ajira na kipato kwa vijana, hasa katika sekta ya uvuvi na ukuzaji viumbe maji.
Akizungumza katika Hafla hiyo Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana, Mhe. Dkt. Joel Nanauka, alikabidhi rasmi mikopo hiyo kwa vijana 308, na kueleza kuwa ni hatua muhimu katika kuwezesha vijana wa Tanzania kushiriki kikamilifu katika uchumi wa buluu, ikiwa ni sehemu ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
Waziri Nanauka ameeeleza kuwa mikopo hiyo itasaidia vijana kuanzisha miradi ya kibiashara kama vile ufugaji wa samaki, ufugaji wa jongoo bahari, kilimo cha mwani, na unenepeshaji wa kaa.
Aidha ameeleza kuwa miradi hiyo ni muhimu kwa kukuza uchumi wa nchi, hasa katika Mikoa ya Mwanza, Kagera, na Mara, ambapo uzalishaji wa samaki unatarajiwa kuongezeka na kuchochea maendeleo katika jamii.
" Rais Samia Suluhu Hassan kwa maono yake ya kutoa fursa za kiuchumi kwa vijana na kuwahamasisha kujiajiri, akisema kuwa Serikali imejitolea kuendelea kutoa rasilimali kwa vijana kama sehemu ya utekelezaji wa ahadi ya Rais ya kutenga Shilingi Bilioni 200 kwa ajili ya biashara ndogo na za kati kwa vijana"Alisema Waziri Nanauka.
Nanauka amesema kuwa Serikali imeweka mifumo madhubuti ya usimamizi wa mikopo ili kuhakikisha miradi inayotekelezwa itatoa matokeo chanya kwa vijana na jamii kwa ujumla.
" vijana kuwa hawa ni wakopaji wa mfano na wanawajibika kuhakikisha fedha hizo zinatumika kwa usahihi na kwamba marejesho ya mikopo yataweza kusaidia kutolewa kwa vijana wengine." Alisema Nanauka.
Nanauka alieleza alisisitiza kuwa Programu ya BBT ina manufaa makubwa kwa vijana, kwani inawasaidia kubadili mtazamo wao kuhusu ajira, huku wakijengewa ujuzi wa biashara na usimamizi wa miradi.
"vijana wamejengewa uwezo wa kutekeleza miradi yenye tija kwa ajili yao na Taifa kwa ujumla. Aliwashukuru wadau mbalimbali, ikiwa ni pamoja na Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), kwa ushirikiano mkubwa katika kutoa mafunzo ya ujasiriamali, uwekezaji, na ufuatiliaji wa masoko kwa vijana." Alisema Nanauka.
Akizungumza kwenye hafla hiyo,naibu katibu mkuu uvuvi Mohamed Sheikh amewleza kuwa kuwa Programu ya BBT ni muhimu kwa vijana kwani inawawezesha kuanzisha na kusimamia miradi yao ya biashara, hivyo kuboresha maisha yao na kuchangia katika uchumi wa taifa.
“Programu hii inawawezesha vijana kubadili mtazamo wao kuhusu ajira na kuwawezesha kushiriki kwa nguvu katika shughuli za uzalishaji wa mazao ya uvuvi. Tunataka kuona vijana hawa wakiwa na mafanikio katika miradi yao.” Alisema Sheikh.













0 Comments