Header Ads Widget

MACHINGA WALIA NA BIASHARA ZAO MSIMU HUU WA MVUA

         

NA EASTER KAMETA (UoI)

MATUKIO DAIMA

Machinga mkoani Iringa waeleza hali ya biashara msimu huu wa mvua huku wakitaja kuwa changamoto kubwa wanayopitia katika biashara zao ni ukosefu wa teja.

Akizungumza na Matukio Daima Mussa Ulaya ambaye ni machinga ameeleza hali ya biashara huku akitaja kuwa biashara ni ngumu kwa sasa kutokana na mvua zinazonyesha  bidhaa zina halibika.

"Mvua hizi za mara kwa mara zinakua kikwazo kwani zinapelekea biashara zetu kuwa ngumu pia sisi kukuosa wateja kutokana kwamba watu wengi si wakazi wa mjini hivyo inapelekea sisi kupishana nao pia bidhaa zetu zikinyeshewa zina haribika"


                                            Naye meshack Adison ametaja kuwa kubadilika kwa bei kuanawafanya wao  kushindwa kuendeleza biashara zao  pia suala la mtaji limekuwa kikwazo kwa wao kufanya biashara katika sehemu mbalimbali   .

"Asilimia yetu kubwa kwa sisi machinga hatuna mitaji ya kutosha kwani biashara zetu ni za kutembeza kupanda kwa bei kunatuathili sisi kama wafanya biashara  pia inapelekea kukosa wateja kutokana kwamba inatubidi nasisi kupandisha bei .

Naye Sarome Exavel ameeleza kuwa maeneo waliyo pangiwa hayana wateja wa kutoshua huku  akitaja kuwa pia tatizo la usafirishaji wa bidhaa ni changamoto msimu huu wa mvua.

"Upatikanaji  wa bidhaa ni mgumu kutokana na mvua pia hata uzaji ni mugumu katika eneo tulilopewa kwani hakuna wateja wa kutosha katika eneo hilo hivyo inapelekea sisi kutembeza bidhaa ili kuepuka kuharibika"

Pia Agness ndete ameeleza kuwa kutokana na biashara zake za kuzungusha zinamfanya yeye kupishana na wateja  kutokana na mvua pia kwenda kusimama mahali pasipo na wateja hivyo hufanya biashara kuwa mbaya pia kupungua kwa mtaji.

"Biashara inakiwa mbaya pale ambapo unatembea njiani kuzungusha bidhaa yako unapopishana na mteja kutokana na mvua , mteja anakosa kabisa kukupa ushirikiano kwani naye anakua anakimbia mvua hivyo hufanya mauzo katika biashara kuwa mbaya na kupungua kwa mtaji .

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI