Header Ads Widget

PROF. SHEMDOE KUZIFANYIA KAZI CHANGAMOTO ZA WAFANYABIASHARA SOKO LA MABIBO.


Dar es Salaam

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu - TAMISEMI, Mhe .Prof. Riziki Shemdoe amekutana na kufanya mazungumzo na baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Mabibo kwa lengo la kutatua mgogoro uliopo katika soko hilo.

Akizungumza na Wafanyabiashara hao mapema leo Machi 04, 2026  katika ofisi ndogo za OWM-TAMISEMI Magogoni Jijini Dar es Slaam, Prof. Shemdoe amesema  yuko tayari kutatua changamoto za wafanyabiashara walizoziwasilisha kwake ambazo ni pamoja na kurejeshwa katika soko hilo baada ya kuzuiliwa na uongozi wa soko, kurudishiwa vizimba vya biashara na ombi la kutaka usimamizi wa soko hilo kujeshwa kwa wafanyabiashara wa Mabibo.  

Prof. Shemdoe ameahidi kushughulikia maombi ya wafanyabiashara hao ndani ya wiki mbili na kuwaahidi kukutana tena baada ya kupata ufumbuzi wa suala hilo.

Aidha, Prof. Shemdoe ameteua kamati Maalum ya kushughulikia suala hilo chini ya uenyekiti  wa Naibu Katibu Mkuu anayeshugulikia Miundombinu  Mhandisi Rogatus Mativila.   

Hatua  ya Prof. Shemdoe inafuatia maelekezo aliyoyatoa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Mwigulu Nchemba  baada ya wafanyabiashara hao kuwasilisha changamoto hizo kwake.





Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI