📌 WAZIRI GWAJIMA KUTOA TAARIFA YA TANZANIA
Na WMJJWM- New York Marekani
Nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa zimekutana Jijini New York nchini Marekani kwa lengo la kujadili hali ya Wanawake katika nchi hizo.
Mkutano huo ni wa 70 kuhusu Hali ya Wanawake Duniani unaoongozwa na Kaulimbiu isemayo "Kuhakikisha na Kuimarisha upatikanaji wa Haki kwa Wanawake na Wasichana wote, ikiwa ni pamoja na kukuza mifumo ya kisheria nyenye usawa na jumuishi, kuondoa sheria, sera, na desturi za kibaguzi na kushughulikia vikwazo vya kimuundo", (Ensuring and Strengthening access to justice for all Women and Girls, including by promoting inclusive and equitable legal system, eliminating discriminatory laws, policies, and practices and addressing structural barriers”).
Mkutano huo umefunguliwa na Antonio Guterres Machi 09, 2026 na utamalizika Machi 19, 2026.
Mkutano utajadili masuala mbalimbali ya upatikanaji wa haki na huduma kwa Wanawake ikiwemo haki ya upatikanaji wa Ardhi, haki kwa upatikanaji wa Elimu, haki ya kujua masuala ya sheria na upatikanaji wa haki za kisheria, kushiriki katika masuala ya uongozi na siasa, haki ya kumilili na upatikanaji wa huduma bora za Afya.
Siku ya kwanza ya mkutano huo, Tanzania imeongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Felister Mdemu, Wataalamu kutoka Wizara hiyo, Wizara nyingine za Kisekta, Taasisi za Serikali na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali.
Aidha taarifa ya Nchi katika Mkutano huo itatolewa na Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe.Dkt. Dorothy Gwajima.







0 Comments