Header Ads Widget

MISS WORLD KANDA YA NYANDA ZA JUU KUSINI ATOKA IRINGA ‎

 


‎Mrembo Cylia  Mussa Ng'wani Toka mkoani Iringa ameibuka mshindi katika mashindano ya kutafuta mrembo atakaye wakilishi ukanda wa nyanda za juu kusini kati ya warembo tisa walioshiriki katika mikoa Saba.

‎Mashindano hayo yamefanyika mkoani Njombe huku mshindi wa pili akitokea mkoani Njombe Miss Aneth Mwakyusa Toka kitengo Cha habari na mawasiliano Halmashauri ya mji wa Njombe

Akimvisha taji la urimbwende mrembo huyo Mbunge wa viti maalum mkoa wa Njombe Kupitia Chama Cha ukombozi wa Umma Sigrada Mligo amewataka wazazi kutobeza vipaji vya watoto kwani mashindano ya urembo kwa sasa ni kazi kama kazi nyingine na yanaingiza Pesa.


‎Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Njombe Erasto Mpete amewataka wazazi kuwaruhusu watoto Kushiriki katika mashindano ya umiss kwani hivyo ni vipaji Wala  sio uhuni.

‎Naye Mratibu wa mashindano ya urembo  nchini Tanzania Benedict Msofe amesema hawaangalii uzuri wa sura pekee bali elimu,akili na miradi wanayofanya ili kuleta mabadiliko chanya katika Jamii.

‎Dorcas Francis mkurugenzi wa Miss World Kanda ya Nyanda za juu kusini anasema  mikoa Saba imehusishwa kwenye shindano Hilo hivyo washiriki wote tisa wataingia mkataba wa Mwaka Mmoja kufanya kazi kutokana na andiko la mradi walilonalo huku mshindi wa kwanza na wengine wawili watakwenda katika Hatua ya mashindano Kitaifa.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI