Header Ads Widget

MAGEREZA YASEMA MAHAKAMA MTANDAO IMESAIDIA KESI KUSIKILIZWA KWA WAKATI

 


Askari zaidi ya 400  wamepandishwa vyeo vya kopro na sajenti


Na Lilian Kasenene, Morogoro, Matukio DaimaApp 


JESHI la Magereza nchini limesema kufungwa kwa Mahakama mtandao kumesaidia watuhumiwa kusikiliza kesi zao kwa wakati.

Kamishna wa utawala na msimamizi wa rasilimali watumwa jeshi hilo kamishna Ahmadi Said Mwen-Dadi alisema mfumo huo pia umesaidia kupunguza gharama za kusafirisha watuhumiwa kwenda na kurudi mahakamani.

"Mahakama mtandao imesaidia suala na ulinzi na usalama kwa wafungwa na watuhumiwa, kupunguza gharama na watuhumiwa kusikiliza kesi zao kwa wakati" alisema Kamishna Mwen-Dadi. 

Akifunga mafunzo na kuwapandisha vyeo askari 422 waliohitimu katika chuo cha Magereza  Kingolwira KPF Morogoro kamishna huyo alisema mahakama mtandao imepunguza usumbufu siyo kwa magereza tu bali hata kwa jamiii hasa wakati wa kuwasafirisha mahabusu kwenda mahakamani na kuwarudisha magerezani.

Kamishna Mwen-Dadi alisema kuhusu suala la kulisha wafungwa na watuhumiwa kila mkoa unatakiwa kuwa na chakula cha kutosha kulisha watu wake walioko kwenye Magereza zao.

Aidha aliongeza kuwa kwa sasa magereza yote nchini pia tayari yanatumia nishati safi na hivyo kucha uharibifu wa mazingira 

Akizungumza kwenye hafla hiyo  mkuu wa magereza mkoa wa Morogoro Kamishna msaidizi mwandamizi Peter Anatory alisema kwa sasa mkoa wake wanajitoshereza kwa chakula kwa asilimia 75.

"Morogoro tuko vizuri kiutendaji, hivi sasa tunajitosheleza kwa chakula kwa asilimia 75 na kwa msimu huu tunajitahidi kujitosheleza kwa asilimia 100," alisema Anatory.







Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI