Header Ads Widget

KIONGOZI MKUU WA IRAN ADAIWA KUFARIKI, TRUMP NA NETANYAHU WAONYESHWA PICHA YA MWILI

 

Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, ameripotiwa kufariki dunia, kwa mujibu wa madai ya maofisa kadhaa wa Israel. Inadaiwa mwili wake ulipatikana chini ya vifusi katika makazi yake nchini Iran kufuatia mashambulizi ya anga yaliyofanywa na Marekani kwa kushirikiana na Israel.


Kwa mujibu wa ripoti, Rais wa Marekani Donald Trump na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu walionyeshwa picha ya mwili wa Khamenei. Kituo cha televisheni cha Channel 12 kiliripoti kuwa, "Picha ya mwili ilionyeshwa kwa Netanyahu na Trump."

Shirika la utangazaji la umma la Israel, Kan, lilieleza kuwa maofisa wakuu wa Israel waliarifiwa kuhusu kuondolewa kwa Khamenei na kwamba mwili wake ulitolewa kutoka kwenye vifusi vya makazi yake. Hata hivyo, hadi sasa hakuna uthibitisho rasmi kutoka Tehran kuhusu kifo chake


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI