Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera
Jamii mkoani Kagera imetakiwa kutilia mkazo suala la lishe hususani kwa watoto ili kukabiliana na udumavu na utapiamulo ambao unaukabili mkoa huo hali inayopelekea kushuka kwa kiwango cha ufaulu kwa watoto na kupoteza nguvu kazi ya taifa.
Wito huo umetolewa na Afisa lishe manispaa ya Bukoba Winfrida Lyoba wakati akitoa elimu ya lishe kwa wazazi na walezi wa wanafunzi wa shule ya msingi Bunena ambapo ameleeza kuwa mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa inayofanya vibaya katika suala la lishe ukiwa na kiwango kikubwa cha udumavu na utapiamulo.
“mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa inayofanya vibaya katika suala la lishe hivyo tunaendelea kutoa elimu ya lishe kwa wazazi kupitia majukwaa mbalimbali ikiwemo mikutano na vyombo vya habari lengo kubwa ni kuhakikisha tunakuwa na Kagera na Bukoba isiyokuwa na udumavu”
Aidha Afisa huyo amewasisitiza wazazi kuchangia chaukula shuleni ili kuwawezesha watoto wao kujifunza kwa urahisi na hivyo kukuza ufaulu wao na kujenga jamii yenye watoto imara kwa manufaa ya jamii na taifa kwa ujumla.
“jamii inatakiwa kuelewa kuwa suala la lishe alianzii ukubwani linaanzia wakati mtoto akiwa tumboni mpaka wakati wa balee, kwahiyo niwasisitize wazazi na walezi kuchangia chakula shuleni ili kujenga jamii bora ya sasa na baadae”
Kwa upande wake Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Bunena Devotha Salvatory amesema kuwa muitikio wa wazazi kuchangia chakula shuleni hapo ni mdogo ambapo kwa kati ya wanafunzi 700 wazazi wanaochangia chakula ni wanafunzi 150 hadi 200 hivyo kuwataka wazazi na walezi kujitoa kuchangia watoto wao chakula.
“muitikio wa uchangiaji wa uji shuleni ni mdogo, shule yetu ina wanafunzi 700 lakini wanochangia chakula ni kati ya 150 hadi 200, bado ni idadi ndongo hivyo nawaomba wazazi kuendelea kuchangia chakula kwa watoto wao”
Aidha Mwalimu huyo amesema kuwa tangu wanafunzi wa shule hiyo waanze kunywa uji shuleni hali ya ufaulu imeongezeka kwa asilimia 90 lakini pia imepunguza utoro kwa wanafunzi.
Naye diwawani kwa kata ya Bakoba Rashid Shabani amesema kuwa katika kuboresha hali ya taaluma katika shule hiyo miongoni mwa suala muhimu la kutilia mkazo ni pamoja na uchangiaji wa chakula shuleni kwa wanafunzi.
“katika kukuza ubora wa elimu katika shule hii tumeona tutilie mkazo suala la uchangiaji wa chakula husasni uji ili kuhakikisha tunaongeza ufaulu kwa watoto wetu kwahiyo tunaamini kuwa kupitia elimu hii wazazi watabadilika na kujitoa kuchangia chakula kwa watoto wao”
Nao baadhi ya wazazi waliopata elimu hiyo akiwemo Amida Malijani ameshukuru kwa kupatiwa elimu hiyo na kuahidi kuendelea kuchangia chakula shuleni huku akibainisha kuwa kikwazo kikubwa kinachopelekea baadhi ya wazazi kushindwa kuchangia chakula kwa watoto wao ni ugumu wa maisha na kuwa kipato kidogo.
“nashukuru kwa elimu tuliyopatiwa uelewa juu ya lishe ulikuwa mdogo kwa wazazi lakini kupitia elimu hiii itasaidia wazazi kuhamasika na kuchangia chakula kwa watoto wao pia kikwazo kikubwa kwa wazazi ni ugumu wa fedha hali ya maisha ni ngumu”
Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa 10 nchini yenye kiwango kikubwa cha udumavu kwa watot ikiwa katika nafasi ya sita kwa asilimia 34.3 ambapo watoto wanne kati ya kumi wanaudumavu.





.jpeg)





0 Comments