Header Ads Widget

DKT. JANEMARY NTALWILA MWANASAYANSI MWANAMKE BINGWA WA UTATUZI WA MIGONGANO KATI YA BINADAMU NA WANYAMAPORI

 

Dkt. Janemary Ntalwila

Kuelekea Siku ya Wanawake Duniani, tarehe 08 Machi, Mwaka huu.

Mwanasayansi Mwanamke anaijulisha jamii kunauwezekano wa Maisha jumuishi kati ya binadamu  na wanyamapori   huku  Swali linabaki  inawezekana vipi binadamu kuishi pamoja na  mnyamapori mkali ?

Huyu ni Dkt. Janemary Ntalwila mtafiti Mkuu kutoka TAWIRI  na mbobezi katika utatuzi wa migongano baina ya binadamu na wanyamapori wakali na waharibifu.

Dkt. Ntalwila anabainisha kuwa sayansi ni dira ya Maisha jumuishi kati ya binadamu na wanyamapori kama vile  tembo,mamba, kiboko, Simba nk ambapo anabainisha  tafiti zimesaidia ahueni kwa wananchi waliokuwa wakipata usumbufu na uharibifu wa tembo, mamba na viboko 


Akigusia changamoto ya Mamba na viboko inayoathiri wananchi waishio pembezoni mwa mito/maziwa Dkt.Ntalwila amesema TAWIRI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imekuwa mstari wa mbele katika ujenzi   wa vizimba maalumu vya kudhibiti athari za  mashambulio ya Mamba na Viboko sambamba na kutoa elimu ya kutumia vizimba hivyo kwa wananchi husika.

Aidha, amehitimisha kuwa utafiti wa kisayansi umesaidia  kurejea kwa hali ya usalama wa maisha ya kila siku kwa wananchi waishio pembezoni mwa mito/maziwa  kuendelea na utamaduni na shughuli zao bila athari za mashambulio ya mamba ambapo hadi sasa serikali  imewezesha  ujenzi wa vizimba zaidi ya 50 katika maeneo yaliyoathirika zaidi: ziwa Victoria, Tanganyika, Nyasa na mito mikubwa ikiwemo Ruvu, Pangani, Kilombero, Ugalla ,Ruvuma n.k.

Ujenzi huu uneenda sambamba na kutoa elimu kwa wananchi wa eneo husika namna ya kutumia na kutunza vizumba hivi.

Dkt. Janemary Ntalwila akiwa 'field' uwekaji wa vizimba vya kuzuia mamba


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI