Na Anold Deogratias Matukio Daima Media Kagera
Wananchi wa Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wameiomba serikali kupitia wakala wa barabara za mjini vijijini TARURA kuzifanyia ukarabati barabara ambazo zimeharibika hasa zilizopo katika ya mji.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti Moza Issack Kabaju amesema kuwa ubovu wa barabara unasababisha kuharibika kwa vyombo vya usafiri kutokana na mashimo yaliyopo kwenye barabara hizo na pia kusababisha ajali.
"ubovu wa barabara hizi unasababisha kuharibika kwa vyombo vya usafiri, magari yanaharibika hapa na wakati mwingine yanasababisha ajali kwa watembea kwa miguu wakati magari na pikipiki wakijaribu kukwepa mashimo haya".
Naye Lameck Wilbard amesema kuwa ubovu wa barabara hizo unasababisha kusitisha shughuli za usafiri na usafirishaji hasa nyakati za mvua kutokana na mashimo hayo kujaa maji, hivyo ameomba kuzibwa kwa mashimo hayo angalau kwa vifusi.
"barabara inajaa maji wakati wa mvua na kusababisha kukatiza shughuli za usafiri na usafirishaji na kuleta adha kwa watembea kwa miguu tunaomba watuwekee hata kifusi"
Akizungumzia barabara hizo Meneja wa wakala wa barabara za mjini na vijijini TARURA wilaya ya Bukoba Mhandisi Emmanuel Festo amesema kuwa serikali tiyari imekwisha mkabidhi mkandarasi barabara hizo zenye urefu wa kilometa kumi ambapo ataanza ujenzi wa barabara hizo hivi karibuni.
"baraba hizo tumeishazipokea na tayari mkandarasi ameishakabidhiwa barabara hizo katika manispaa ya Bukoba zenye urefi wa kilometa 10 na hivi karibuni ataanza ujenzi wa barabara hizo ambazo zimeharibika".
Pia ameeleza kuwa ujenzi wa barabara manispaa zenye urefu wa kilometa 10 zinatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi billioni 21 pesa kutoka benki ya dunia kupitia mradi wa tactics na itajengwa chini ya kampuni ya China ya Shangdong.
Sambamba na hiyo halmashauri ya manispaa ya Bukoba imetenga Bajeti ya shilingi billioni 2.87 kwa ajili ya ujenzi wa barabara nyingine zenye urefu wa kilometa 51, mifereji yenye urefu wa kilometa 1.6 pamoja na madaraja mawili.
0 Comments