Header Ads Widget

TAWA YAZINDUA BOTI YA LUNDO ISLAND TOURS


Na. Mwandishi Wetu, Ruvuma


Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania - TAWA, kupitia Kanda ya Kusini Mashariki, leo Februari 15,2026, imezindua rasmi Boti mpya ya kitalii inayojulikana kama Lundo Island Tours kwa lengo la kuchagiza utalii katika Visiwa vya Lundo na Mbambabay vilivyopo katika Mkoa wa Ruvuma.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa boti hiyo, Mgeni Rasmi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Bridegia Jenerali Ahmed Abbas ameipongeza TAWA kwa jitihada zake za kukuza utalii katika Visiwa vya Lundo na Mbambay.

Ameongeza kuwa ununuzi wa boti ni wa kimkakati katika kufungua fursa mpya za Utalii katika Wilaya ya Nyasa na Mkoa wa Ruvuma kwa ujumla.



Sambamba na hayo, Bridegia Jenerali Abbas amewataka viongozi wa Wilaya na jamii kushirikiana na TAWA katika miundombinu hiyo ya utalii pamoja na bioanuai zote zinazopatikana katika hifadhi hiyo.

Naye, Kaimu Kamanda wa Kanda ya Kusini Mashariki, Khadija Malongo ambaye alimwakilisha Kamishna wa Uhifadhi wa TAWA amesema ununuzi wa boti hiyo ni sehemu ya mpango wa kukuza utalii na kuimarisha miundombinu ya utalii ili kuhakikisha huduma bora kwa wageni wanaotembelea visiwa hivyo. 

Visiwa vya Lundo na Mbambabay ni visiwa vinavyopatikana katika Wilaya ya Nyasa, Mkoa wa Ruvuma na vimezungukwa na madhari nzuri iliyosheheni mimea, Ndege, Wanyamapori, Samaki wa mapambo na fukwe zenye maji angavu.




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI