Pwani, 10 Februari 2026
___________________________________
Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) imeendesha mafunzo maalum kwa wamiliki wa viwanda mkoani Pwani, yakilenga kuhamasisha matumizi ya Nembo ya Taifa – Made in Tanzania Brand. Mafunzo hayo yalifanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani na yalihudhuriwa na washiriki 85 kutoka viwanda mbalimbali.
Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Bi. Rehema Akida alisisitiza umuhimu wa Watanzania kujivunia bidhaa zao na kutumia Nembo hiyo kama nyenzo ya kushindana kimataifa. Alipongeza TanTrade kwa juhudi zake za kutambulisha bidhaa za Tanzania na kuunganisha wazalishaji wa ndani kupitia rajam hiyo.
Kwa upande wake, Bw. Boniface Mrema – Meneja wa Kitengo cha Kujenga Uwezo na Huduma za Ushauri (MCBAS), akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade, alieleza kuwa lengo la Nembo hiyo ni kuendana na kasi ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kulea na kusaidia wazalishaji wa ndani.
Alitoa wito kwa wazalishaji kuchangamkia fursa hiyo, akisisitiza kuwa Made in Tanzania Brand ipo mahususi kwaajili ya kuinua ushindani na hadhi ya bidhaa za Tanzania katika soko la Ndani na Kimataifa


















0 Comments