Na. Matukio Daima Media, Dar es salaam.
KLABU ya 'Wekundu wa Msimbazi' Simba SC ya Jijini Dar es salaam, imeingia mkataba na kampuni ya Mainstream Group na Nexus Pesa kuwatengenezea kazi za Uanachama ambazo zitaanza tolewa mwezi Machi 27 mwaka huu.
Hayo yamebainishwa leo February 10, 2026 na Uongozi wa Simba SC mbele ya Waandishi wa habari wakati wa tukio la utambulisho wa Mkataba huo na kampuni hizo mbili.
"Leo tumekusanyika hapa kwa jambo la muda mrefu ambalo limesubiriwa sana. Tulikuwa tunatafuta kampuni ya uhakika kutengeneza kadi za Simba, kadi za uanachama ambazo zinafanana na timu kubwa kabisa Afrika."
"Bodi ya Wakurugenzi inapenda kuitangaza kampuni ya Mainstream kuwa ndio itatengeneza mfumo wa kileo na za kisasa na imeichagua kampuni ya Nexus kutoa kadi hizi za wanachama. Kadi hizi zitakuwa aina ya VISA.”
"Hii inakwenda kuwa Visa card pamoja na kukutambua kwamba ni mwanachama wa Simba lakini pia unaweza kuweka pesa, ukafanya malipo na miamala."- Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Crescentius Magori.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi na Mwenyekiti wa Klabu, Murtaza Mangungu amesema:
"Tumeingia mkataba na wenzetu Mainstream Group na Nexus Pesa, utoaji wa kadi za uanachama utafata katiba ya Simba kuanzia ngazi ya matawi hadi ngazi ya makao makuu ya klabu.
Ni wakati muafaka kwa wanachama hasa kwenye ngazi ya matawi na tutaanza usajili wa matawi hivi karibuni."
"Tumepanga kuanza kutoa kadi tarehe 27 | Machi / 2026.
Tunafanya hivyo sababu kuna mambo mengi na kuna taasisi nyingi zinahusika katika maandalizi ya utoaji wa hizo kadi."- amesema Murtaza Mangungu.











0 Comments